Friday, January 20, 2017

Published 1/20/2017 06:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-15




ILIPOISHIA…
Machozi yalianza kunilengalenga tena na kujikuta nikianza kulia kwa kwikwi ila kilio chenye uchungu na hasira ndani yake. Niliendelea kulia hadi muda wa Maiko wa kutoka kazini, akawa amerudi na kunikuta nalia.
SONGA NAMI…
“Eeeh na wewe unalilia nini.”
 “Amna, kawaida tu!”
 “Kawaida gani hiyo huku  unapigia watu kelele na nguo umezilowanisha kwa machozi, ebu sema huko nini kinakuliza,” aliniuliza kwa ukali.

Nilimsahngaa sana kuniuliza kwa ukali kana kwamba anajua kila kitu kilichotokea, nilimsimulia Maiko kila kitu kilivyokuwa, niliamini kama kijana angepata wasaha wa kujiuliza kisha kuchukua hatua. Lakini alichofanya ni kuniambia kuwa inawezekana nilimjibu vibaya mama yake, ndiyo maana akaniambia maneno yale kwa hasira.

Majibu ya Maiko hayakuiniingia akilini bali ilinibidi nikubaliana naye kwa shingo upande. Siku ikaisha, nikijua kesho mama mkwe atakuwa amepunguza jazba na pengine tutaongea vizuri lakini cha ajabu kulipokucha hali ikazidi kuwa ileile na tena siku hiyo iliongezeka, mama anaongea hadi povu linamtoka mdomoni.
Kama bile sijazaa na mtoto wake, hata kama nimekosea mama Maiko ni kama mama yangu, kwa nini basi asingeweze kuniita na kuzungumza nami kwa upole, nilijiuliza sana bila kupata chanzo cha ukorofi ule.

Nikiwa bombani nafua mama mkwe alipita akielekea maliwatoni nilikuwa ninafua, nilimsalimia lakini hakuitikia, niliumia sana, nikarudia tena lakini wapi, hakujibu. Nilikaa kimya ila moyo wangu ulikuwa una maswali mengi sana juu ya maisha ya hapo nyumbani kwao Maiko.
 
Nilifikiria sana juu ya maisha ya mwanamke na kugundua kuwa sehemu kubwa ya maisha ya mwanamke ni kama yamejaa mateso zaidi kuliko furaha, kwani kupata mwanaume mkweli na mwenye mapenzi ya dhati ni mara chache na ni bahati kubwa, kama kupata kwa jua kule kullikotokea mkoani Mbeya.

Nili kilifuatika katika maisha yam dada Kecho na mwanaye ukweni? Usikose kesho muda kama huu.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
      edit