Karibu tena katika
kujuzana kuhusu elimu ya mahusiano na mada ya leo itazungumzia namna ya
kurudisha mahusiano yako ili yawe mapya
Inashangaza kwa baadhi ya wapenzi
kujifanya wao ni miamba katika uhusiano kwa kushindwa kuomba msamaha kwa kuona
kama ni kujidhalilisha mbele ya wapenzi wao, jambo ambalo halina ukweli wowote.
Kama wanadamu, kila mmoja
ameumbwa na udhaifu wake, ingawa pia kuna wengine wamekuwa wakiutumia msemo huo
kufanya makosa kwa kusudi.
Kama utafanya jambo kwa
kujua kuwa ni kosa na wewe ukatenda kwa vile msamaha upo, ni dhahiri kabisa
kuwa neno msamaha halitakuwa na maana hiyo.
Watu hufikia hatua ya
kugombana pale wanapotofautiana kauli, mitazamo na kadhalika kwa maana ya kila
mtu kuwa na mtazamo au kauli yake. Ili kuweza kukubaliana ni lazima mmoja wao
akubali kauli au mtazamo wa mwenziye ili maisha yasonge mbele na kama kila mtu
anataka jambo lake likubalike basi hapo ndipo unapozuka mvutano.
Kama wote mtakuwa juu na
hakuna mmoja wenu anayekubali
kujishusha au kukubaliana na wazo la mwenzi wake,
hakika hakutakuwa na suluhu yenu ni lazima mmoja ajifanya mjinga. Ingawa usiwe
siku zote mjinga kwani utaonekana unapelekwa kwenye ukweli, mwambie mwenzi wako
ukweli hata kama atabisha usoni ila moyoni ukweli wako utamsuta tu.
Inawezekana mkawa
mmekwazana na kuumizana sana kwenye uhusino wenu, kama unahitaji kurudisha
furaha ya ndoa au mapenzi yenu baada ya kukosana, fanya yafuatayo;
JISHUSHE
Lazima mmoja wenu akubali
kujishusha au kujifanya mjinga mnapohitilafiana ili kupata suluhu lakini kama
kila mtu atakuwa mbogo, hakika hamuwezi kufika kokote muendako. Maisha ni
kupambana na kuvumiliana, hakuna uhusiano usiokuwa na migongano.
KUKUBALI MAKOSA
Ni lazima ujifunze
kukubali makosa pale unapokosea, kila mwanadamu ana upungufu wake, haiwezekana
wewe ukawa ni mkamilifu siku zote. Kila ukikosea unakataa na kuingiza mfumo fulani
wa kijeuri ndani yake, maisha hayaendi hivyo, jifunze kukubali makosa.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U