Saturday, January 14, 2017

Published 1/14/2017 03:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA!-9




NILIPOISHIA…
Mama aliendelea kunisisitiza kusukuma kwa nguvu, nikawaza nilivyomsumbua mama yangu kisa kikiwa ni raha zangu na Maiko, nikajikuta nasukuma mtoto kwa hasira.

ENDELEA NAMI…
Mama akampokea mtoto na kumfuta hatimaye, nikasikia sauti ya kichanga kikilia, ng’a ng’a ng’a ng’a nikasahau hata maumivu yale ya kusukuma nikamwambia mama namuomba mtoto wangu, nikiwa nashauku kubwa sana ya kumbeba, mama ananiambia nisubiri kwanza amsafishe mtoto, akafanya hivyo kisha akamuweka pembeni na kuanza kunisafisha mimi pia.

Basi mama akanikabidhi mtoto wangu, nikakimbisu, kilikuwa ni kitoto cha kike, nilifurahi sana, wakati huo kitovu kilikuwa kinaning’inia tu.
Hatukuwa na namna zaidi ya kuanza safari ya kurudi nyumbani huku nikitembea taaratibu. Ilibidi nijikaza tu kwa safari hiyo kwani ni kama tulikuwa tumefika nusu ya safari ya kwenda zahanati au kurudi kijijini, kwetu ikawa bora kurudi kijijini.

Hatimaye tulifika, mama akaingia jikoni na kuchemsha maji ya moto akaanza kunikanda wakati huo akiwa ametengea chungu cha uji, alipomaliza kunikanda akanipa uji, nikaanza kunywa, nikukweli nilikunywa sana kwani tumbo nililoona kama lina nafasi kubwa kuliko nilivyokuwa na ujauzito.

Baada ya siku tatu baba akawa amefika pale nyumbani na kukuta nikiwa nimjifungua, hakuwa na msaada wa kitu chochote kwani kuna wakati hata pesa ya kula alikuwa aachi na hivyo nilijikuta nikishinda njaa.


Kushinda njaa kwa kuwa ilikuwa ni sehemu ya maisha yangu niliyokulia, haikuwa shida sana ila shida ni kuwa nimetoka kujifungua na nilipaswa nile nishibe ili nipate maziwa ya kunyonyesha mwanangu lakini hakuwa hivyo kwa hiyo nilipopata nilikula nilipokosa nilishinda au kulala njaa.

Miezi mitatu ilipita bila mtoto kupewa jina, akaendelea kunisumbua sana ikiwa mtoto ni wa kulialia tu mara kuugua, nikaamua kwenda tena kule center kwa jili ya kumtafuta Maiko kwenye simu.
Kecho alifanikiwa kumpata Miako kwenye simu baada ya kufika center?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit