KARIBU sana mpenzi msomaji wa makala haya, ni siku
nyingine tena kwa kudra za Mwenyezi Mungu tunakutana kwa ajili ya kuelimishana juu
ya uhusiano.
Na kwenye mada ya leo nitazungumzia kuhusu mtu mwenye
mpenzi anashindwa kupata faraja kwa mpenzi wake ambaye amevurugwa kazini na
alitegemea akifika nyumbani mpenzi wake atamsaidia kuondoa hizo stress lakini
matokeo yake nyumbani nako inakuwa ni ni
mateso bila chuki ni stress zaidi.
Msongo wa mawazo au stress ni tatizo kubwa sana kwenye
uhusiano wowote ule, uwe wa kirafiki, kimapenzi na kadhalika. Na msongo huo
unaweza kuchangiwa na mambo mengi sana lakini kikubwa ni mtindo wa maisha ambao
mtu, watu au jamii f’lani inaishi kwa maana ya ugumu na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku .
ingawa mshongo wenyewe unaweza kuwa wa kusababishiwa au kujisababishia
mwenyewe.
Na ili kuondoa msongo wa mawazo mhusika anatakiwa
kukaa sehemu iliyotulivu na kupumzika kwa muda ili kuondoa kilichostresisha na
kuingiza kitu kipya kabisa katika akili na mwili wake.
Napata wakati mgumu sana kuona mpenzi wako ambaye
alitarajia kuwa kimbilio lake, farijiko la moyo wangu, furaha ya moyo wangu
tabibi wa maradhi yangu yanayonisibu kila siku, kila kukicha kila mara naye
anageuka stress kwangu yaani nilitegema kwa kuwa nina stress za kazini basi
nikifika nyumbani mpenzi wangu atakuwa sehemu kubwa sana ya kunilainisha na
kuniondolea stress lakini cha ajabu yeye pia ni sehemu ya kuniongezea hizo
stress.
Iko wapi furaha ya mimi kuwa na mpenzi, iko wapi raha
ya kuwa na mtu kwa ajili ya kunifariji na kuniliwaza wakati napokuwa
nimevurugwa, yuko wapi mpenzi wangu ambaye nilitegemea awe msaada kwangu
napokuwa nimekwama kifkra, ninapokuwa nimekwama kimtazamo, kibinadamu na
mengineyo.
Siioni furaha ya kuwa kwenye uhusiano maana nikiwa
kazini ni stress nikitoka na jua mpenzi wangu nyumbani ataondoa stress za
kazini lakini cha ajabu anakuwa mtu wa kuniongezea stress.
Je, ni kweli sina bahati, ni kweli nilikosea kuchangua
mwenza wa kuishi naye, ni kweli mpenzi niliyenaye si sahihi kwangu, na kama
siyo yupi sasa ni sahihi na ninaweza kumjua kwa mtindo upi, je, nitampata wapi?
Kanisani, msibani, ngomani, gulioni, sokoni, shuleni,
tamasha, shambani, au sehemu gani? Kwa mtindo huo wa kustresika kila sehemu,
kila wakati nawezaje kufanya faragha yangu kuwa nzuri na bora, nawezaje
kumridhisha mpenzi wangu ili afurahie tendo hilo.
Bila shaka wewe ni mmoja wa wale ambao umewahi
kukutana na suala hili, maumivu haya na kukaona kama vile huna baahati na
mapenzi pasi unaweza kunitumia maoni yako.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U