Friday, January 27, 2017

Published 1/27/2017 12:00:00 PM by

KISA MAHARI, NIMENYANG’ANYWA MKE!



Mimi ni kijana wa miaka 21, nilibahatika kuwa na mahusiano na binti mmoja kiaina lakini nilijitahidi nikapeleka mahari nusu kwao ili niwe na uhalalai wa kummiliki huyo binti kama mke wangu.


 Nashukuru ilipokelewa ile nusu mahari na wazazi wake, nikaendelea kuishi na mke wangu ambaye kwa sasa tuna mtoto mmoja. Cha ajabu hivi karibuni wazazi wake na mke wangu walikuja na kumchukua binti yao kwa madai kuwa sijamaliza mahari.

 Nilishangaa sana kwa kweli, hata kama nimeshindwa kumaliza mahari ndiyo ninyang’anywe kwali mke wangu tena ana mtoto ila nikionana na mke wangu anadai niende kwao nikamchukue.

 Sijui nini chakufanya, pengine wadau  wa M&U mnaweza kuwa na ushauri mzuri zaidi. Naombeni maoni na ushauri wenu kwa wingi zaidi.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit