Thursday, January 26, 2017

Published 1/26/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-21



NILIPOISHIA….

Mawifi waliingia ndani na kunikusanyia kila kilichokuwa changu na kunitupia nje, nililia sana. Wakaanza kunisukuma huku wakiniambia nikamchukue na kidudu washa wangu (mwanangu Gift). Nilishangaa wifi mkubwa aliingia ndani ambapo mtoto alikuwa amelala akamuamsha na kumbeka kisha kuja kunitupia.
ENDELEA NAMI….


Sikuwa na namna ilibidi nikubaliane nao na kuanza kuondoka, huwezi amini nilifukuzwa mbele ya majirani tena jua kali, ambalo lilimchoma vibaya mwanangu, kwani sikuwa na mwamvuli wa kuweza kumkinga mwanangu na jua lile, (anaanza kulia kwa sauti ya kwikwi), kama walikuwa hawanitaki mimi niolewe na ndugu yao, vipi kuhusu damu yao, Gifti, nina uhakika wa asilimia zote kuwa ni damu halisi ya Maiko, au wanataka niwalele na kuwakuzia kisha baadaye waje waseme ni damu yao nwahitaji kumsomesha na kumtunza,  nilishangaa sana unyama wa familia ile.

Nilianza kuondoka taaratibu huku akilini mwangu nikiwaza na kuwazua namna ambavyo nitakutana na ugumu wa maisha, nilipojaribu kumpigia simu Maiko, simu yake ilikuwa bize muda wote, sikuwa na jibu la nini chakufanya zaidi ya kuondoka tu, kwani kazini kwake Maiko sikuwa napafahamu, hata kama ningekuwa napafahamu kwa jinsi ambavyo amekuwa akinijibu ni dhahili naye anahusika katika mpango huo wa kunitimua kinyemela. 

Kwani pamoja na kumueleza mara kwa mara juu ya changamoto na mambo ambayo ndugu zake wamekuwa wakinifanyia lakini bado hakuwa na msaada wowote kwangu zaidi ya kunikandamiza mimi na kunipiga tu kwa madai kuwa nataka kumtenganisha na mama yake, eti mimi ndiyo nitakuwa mkorofi na siyo ndugu zake.

Niliondoka saa 7 mchana jua kali, hata chakula cha mchana sija, majirani karibu mtaa mzima walitoka nje kunitazmani kwani nilifukuzwa kama mbwa tena kwa sauti kubwa sana,  na maneno ya kejeli eti mimi mwanahizaya nalazimisha kuingia kwenye ukoo wao.
 
Taratibu niliondoka katika nyumba ile huku majirani wakiniangalia wengine wakinionea huruma kwa jinsi nilivyofukuzwa kama mbwa, ningawa wengine walinishangaa sana kutaka kuolewa katika familia ile kwani kwa wakati wa mtaa ule wanaifahamu vyema. Na pengine ndiyo maana Maiko akaja kuniokota mimi wa Pwani.

“Nilijifunza kitu, mapenzi yakukutana tu mitaani na kuchukuana ni mabaya sana laity kama ningelijua hilo mapema nisingekubali kushirikia naye tendo la ndoa ningemchunguza zaidi ya vile nilivyomchunguza pengine ningegundua kitu.

“Lakini ndiyo tayari nimeishaliwa, sina namna, nihesabu fungu la kukosa nikaanze maisha mapya kuliko kuendelea kuteseka, kama wameweza kumtafutia mke mtoto wao watashindwa kweli kunipa sumu kwa sababu namng’angania mtoto wao. Kama ni umaskini nimezaliwa nao, acha niendelee kuwa nao tu,”nilizidi kuwaza kichwani.
“Samahani dada eti……

Je, ni kitu gani Kecho anataka kuuliza na mdada mpita njia?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785 

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
      edit