Habari zenu wanaM&U, mimi ni msichana wa miaka 21,
nina mpenzi wangu ana miaka 24 ambaye nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda
wa mwezi 1 sasa.
Yeye ni mtumishi wa afya katika moja ya hospitali
maarufu hapa jijini, kila nikitaka kukutana naye anadai kuwa yuko bize sana,
pamoja na kuwa bize huko lakini pia hata kunijulia hali kwa kunipigia au
kunitumia SMS hafanyi hivyo.
Nimejaribu kumwambia anasema kuwa haitaji kuwasiliana
na mimi kila muda anasema namsumbua.
Nimeumia sana kama mwanamke ambaye ninamkpenda na nimejitoa kwake, sili,
sdilali, siwezi kufanya kitu chochote kwa ajili yake.
Siku moja aliniomba hela kiasi cha Sh. 50,000/= nilikuwa sina, nikamwambia, sasa sijui kama
alikasirika kwa sababu sikumpatia hela au laha, lakini tangu siku hiyo hajawahi
kukaa chini na mimi kuzungumza chochote juu ya mahusiano yetu.
Binafsi nampenda sana niliwahi kumwambia akajitambulishe
kwetu anasema muda bado, cha ajabu kwa sasa hataki kunisikia wala nisiende
nyumbani kwake bila taarifa, nimejaribu kumwamba msamaha lakini hataki
kunisamee anasema hadi siku akiwa na furaha ndiyo atatoa msamaha wake.
Ndugu zangu natesekana sana juu ya huyu mwanaume,
naombeni ushauri wenu ambao utanifungua akili, bado nampenda na ninatamani
kuendelea kuwa naye, nahitaji kurudisdha furaha ya moyo wangu kama mwanzo.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Na.M&U