Habari za leo! Nimshukuru Mungu kwa kunikutanisha nanyi
tena siku ya leo. Niwape pole wale wanaougua au kuuguza ndugu, jamaa, rafiki au
wapenzi wao. Hakika hayo ndiyo maisha
yetu ya kila siku. Ila kikubwa ni kushukuru Mungu kwa kila jambo, pongezi kwa
wale aliosherekea siku ya mama duniani ambayo inaadhimishwa leo lakini pole kwa
wote ambao wamewapoteza wazazi wao. Mungu yuko nanyi siku zote mpaka mwisho wa
hadhari.
Mada ya leo katika ujasiriamali nitazungumzia namna ya
kuijua kazi nzuri ya wewe kufanya katika maisha yako yaliyobaki duniani.
Naweza kusema kumekuwa na janga kubwa sana la watu
kushindwa kufanya kazi ambazo wanazipenda kutokana na mtindo wa maisha au
mashinikizo ya watu wao wa karibu, jambo ambalo linapelekea watu hao kufanya
kazi kwa kiwango cha chini kwa sababu tu si changuo lake.
Wengi wamekuwa wakifanya kazi ambazo hawazipendi kwa
sababu tu ya kudhani pengine zina malipo makubwa, za kistaarabu, kutokujitambua
au kufanya kazi hizo kutokana na matakwa au mashinikizo ya wazazi, mlezi/walezi
au mfadhili ambaye anaishi naye au ambaye anamsomesha.
Kuna jambo kubwa sana la kujifunza kwa wazazi walio na
watoto au wazazi wanaotarajia kupata watoto kwa maana ya kuwapa haki watoto wao
kwa kuchagua kile wanachokipenda katika maisha yao.
Kwa kufanya hivyo unakuwa umempa nafasi ambayo ni sehemu
kubwa ya furaha yake ya maisha yake yaliyobaki chini ya jua.(angalizo, muongozo
kwa kazi husika au jambo husika ni mzuri sana na simaanisha kumuunga mkono
mwanao kwa kazi au tabia zenye uovu).
KAZI NZURI NI IPI?
Ni ile ambayo mtu anaifanya kwa sababu anaipenda kutoka
moyoni mwake, yuko tayari kufanya hata kwa kujitolea, muda, akili na mali yake
ilimradi amefikia au ameishi katika ndoto yake.
Kama mtu akifanya kazi ambayo anaipenda ni dhahiri hawezi
kuchukia hata kama atahitajika usiku wa manane kwa ajili ya kazi yako, yuko
tayari kuwasaidia wahitaji wa kile wanachohitaji katika muda muafaka.
Hachoki kufanya kazi ni kwa sababu tu anaamini anafanya
kitu ambacho amezaliwa kukifanya. Kazi hiyo nzuri kwa mhusika inaweza kuwa ya
kuzaliwa nayo kwa maana ya kipaji au kujifunza kwa maana ya kusomea.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745.
Pia
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U