Mimi ni binti nina miaka
24, nilikuwa na mahusiano ya kirafiki na
kaka mmoja ambaye ni mfanyakazi wa benki moja hivi, baadaye tukawa wapenzi, akaniuliza kama
nampenda kwa dhati au nina mtu mwingine, nilimjibu kuwa sina mtu mwingine zaidi
yake.
Siku zikapita, kuna siku
moja alinipigia simu majira ya saa moja usiku na kuomba nikaonane naye, sikuwa
na wasiwasi nilifunga safari hadi nyumbani kwake.
Tuliendelea na mazungumzo
ya kawaida ikafika sehemu akaniambia kuwa ana hamu ya kufanya mapenzi na mimi,
kwa kuwa nilimpenda sikukataa, nikamkubalia tukaingia kwenye uwanja wa
masumbwi.
Lakini tangu siku hiyo
nilipompa penzi langu mara moja akawa haeleweki, kila nikimtafuta anasema yuko
bize hata kama nikimwambia nina hamu ya kukutana naye faragha anasema kuwa
nisubiri kwanza yeye yuko bize akipata nafasi atanitafuta.
Nimebaki njia panda, nini
tataizo langu, nini kilichomsibu, au kipi alichokutana nacho cha ajabu kwangu kiasi
cha kutotaka kurudiana nami!?
Kusema na ukweli mapenzi
yananitesa sana kwani nampenda sana huyo kaka, sijui hata nifanyeje? Naombeni
msaada wenu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U