Nimshukuru Mungu kwa
kunihurumia pamoja na makosa yote ninayomtendea kimawazo, matendo na hata
kufikiri lakini kwa kuwa ALLAH ni mwenye
rehema bado naishi.
Bila shaka hata na wewe
msomaji ambaye unasoma Makala haya ya ujasiriamali, mshukuru Mungu kwa sababu
kakupa nafasi ya kujifunza kwa hiki ambacho amenipatia. Mimi wala wewe si bora
kuliko wengine ambao wametangulia mbele ya haki, wanaoumwa, wanaoteswa na
mapenzi, maisha na kadhalika.
Mada hii inzungumzia namna
ambavyo unapaswa KUJIKUBALI KWA JINSI ULIVYO bila kujali mapungufu, changamoto,
misukosuko na chochote kile unachokutana nacho.
ISHI kwa kujiamini, jikubali
haswa kuwa wewe ni mtu wa thamani mbele ya uso wa Mungu na hata ukapewa nafasi
ya kuweza kuwapo katika uso wa dunia
hii. Haijalishi changamoto unazokutana nazo chini ya jua. Bado unaweza kushinda
na kuwa mshindi.
Nasikitika sana kuona mtu
anakuwa ajiamini, ajithamini kwa kile kipawa alichojaliwa nacho, Mungu kakupa
kitu hicho kwa sababu maalumu ila kwa sababu ya kutokujiamini hujajua umepewa
au umekuwa hivyo kwa sababu gani.
Tafakali kwa mara nyingine
wewe ni nani, uko duniani kwa ajili ya kufanya nini, na kipi Mungu kakupa
ambacho kina utofauti na wanadamu wengine. Kama umekigundua unasubiri nini
kuanza kukifanyia kazi ili kujinasua hapo ulipo.
Hata kama umepewa ulemavu,
jiangalie unaweza kufanya nini kwa kutumia ulemavu wako ulio nao, yawezekana
umepewa ulemavu ila kichwani uko vizuri sana, kuliko mtu aliyekamalika viungo
vyote, unaweza kubuni au kuchora ramani za nyumba na vitu mbalimbali kwa uzuri
zaidi lakini umebaki kulia na kuwa wewe ni mlemavu. Achana na hayo mawazo
ulinyiwa kiuongo hicho ila ukapewa maarifa. Basi yafanyie kazi.
Yawezekana ulipata ajali
ambayo imekufanya umepooza sehemu ya mwili wako lakini kama kichwa kipo na akili
yake haijapooza piga kazi fikiria kutokana na ulivyo inawezekana kufikia jambo
Fulani.
Unaweza kufikia malengo
yako bila kujali changamoto na magumu yote unayoyapitia, kwani magumu hayo
yamewekwa ili kukufanya ufikie mafanikio.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U