Sunday, January 22, 2017

Published 1/22/2017 10:00:00 AM by

UCHUUZI WA MBOGAMBOGA NA MATUNDA

Wajasiriamali wenzangu karibuni tena katika safu yetu hii ya Ujasiriamali. Baada ya kutumia wiki kadhaa kujifunza kuhusu biashara ya mnadani, wiki hii nawakaribisha katika somo la uchuuzi wa bidhaa ya mbogamboga na matunda.


KWANZA, UCHUUZI MAANA YAKE NINI?
Uchuuzi ni kitendo cha kununua bidhaa fulani kwa bei ya jumla na mnunuzi kwenda kuuza kwa bei ambayo mwisho wa siku atatengeneza faida.
Kwa hiyo ninapozungumzia uchuuzi wa mbogamboga na matunda nazungumzia bidhaa kama mchicha, biringanya, pilipili hoho, karoti, maembe, machungwa, maparachichi, tikiti maji, ndizi na kadhalika.
Biashara hii ni maarufu sana duniani kote kwani nchi nyingi zina wachuuzi wa namna hii. Hata hapa nchini wachuuzi ni wengi sana maeneo ya jijini la Dar, Arusha Mwanza, Mbeya, Tanga na sehemu nyiingine za mijini.

Biashara hii ni sehemu kubwa sana ya ajira za vijana na akina mama walio wengi. Akina mama wengi ambao wako  kwenye matatizo ya kifamilia au wametelekezwa na waume zao, biashara hii imekuwa mkombozi kwao, kwani imeweza kuwasidia kujikimu na hata kusomesha watoto wao kwa biashara hiyo ya kuchuuza mbogamboga na matunda.

Uchuuzi wa mbogamboga unaweza kuufanya kwa kwenda sehemu wanapooza jumlajumla au wakati mwingine unaweza kwenda kwenye mashamba ya mbogamboga kisha ukanunua mboga kwa bei ya jumla na rahisi. Kama ukifanya hivyo kwa mzigo wa mboga wa shilingi 20,000, unaweza kwenda kuupanga upya na kupata mboga zenye kukupatia shilingi 30,000 na kuendelea.
Huanzishaji wa biashara hii hauhitaji mtaji mkubwa sana kwani kwa kawaida mafungu huanza kwa kuuzwa shilingi 100 na kuendelea. Kwa hiyo ni kiasi kidogo sana cha mtaji unaweza kujipanga kuanza nacho hata sasa.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U

      edit