Saturday, January 7, 2017

Published 1/07/2017 10:00:00 AM by

NAITAJI NIJITEGEMEE ILA SIJUI PA KUANZIA, NAOMBA USHAURI



 
Ninaitwa Hawa, ni mdada wa miaka 24, mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya, nilizalishwa na mwanaume wangu mtoto mmoja ili sikubahatika kuishi naye kama mume na mke, naishi kwetu na mama yangu pamoja na wadogo zangu.

Nimepata mwanaume mwingine ambaye niko naye kwa muda mrefu kidogo, nashukuru mwanaume huyu ananihudumia kila kitu mimi na familia yangu, pamoja na kumsomesha mtoto wa mwanaume mwenziye.

Kuna kipindi mwanaume wangu aliniambia nitoke nyumbani ili nikajitegemee nikamwambia muda bado ila kwa sasa nahisi ni muda muafaka baada ya kupata kazi kwenye shirika fulani ambapo kila wiki wananilipa sh. 37000/=

Kwa upande wangu mimi nina vyombo, kitanda, kabati la nguo na jiko, ina nashindwa kujua ni wapi nianzie kwenda kupanga, na kama nitaamua kujitegemea ni kipi cha kuanza kabla ya vingine.
Asante , ninaamini M&U HAMJAWAHI KUMUANGUSHA MTU KATIKA USHAURI.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na:M&U
      edit