Wednesday, January 11, 2017

Published 1/11/2017 03:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA!-6



NILIPOISHIA…
Nilizidi kuumia kutokana na maneno ya wanakijiji hasa wakiwemo wanaume ambao waliwahi kunitaka  kimapenzi, mwili ulianza kudhoofika kwa sababu ya mawazo, nikijiona kama mkosaji sana.


Miezi kadhaa ilipita huku Maiko akiwa hana msaada wala mawasiliano yoyote na mimi pamoja na kumwambia kuwa nilikuwa na ujauzito wake. Niliendelea na maisha yangu pale kijiji, huku maisha yenyewe yakiwa ni ya shida na kubangaiza kwa wingi, sikuwa na namna nilikuwa nimeachwa.

Siku za kujifungua zilizidi kusogea huku nikiwa sina akiba yoyote ya pesa wala vifaa kwa ajili ya kujifungulia, nilizidi kuumia sana, niliona kama dunia inazidi kunielemea.
Kuna wakati mama alikuwa akipata wakati mgumu sana wa kunibembeleza kutokana na kunikuta nikilia mara kwa mara.

Namshukuru sana mama yangu kwa kunitia faraja katika kipindi chote kigumu ingawa hata yeye maisha yake yalikuwa ni magumu sana kwani niliona baba wa kambo alivyokuwa anamfanyia mama yangu mzazi.

Nilifika sehemu nikaamini akilini mwangu kuwa akili na tabia za wanaume wote duniani ni zilezile.
Kuna kipindi nilianza kuhisi kama tumbo linanisumbua, na wakati mwingine nyonga zilikuwa zinabana sana, kiuno nacho kinauma kweli kweli.
 
Sikuwa na namna zaidi ya kuvumilia maumivu yote yale huku nikiomba Mungu kuninithuru na makubwa zaidi, yote hayo ni kutokana na kukosa pesa kwa ajili ya kunipeleka hospitalini ambapo kutoka kwetu kuna umbali kidogo.

Kuna siku hali ilikuwa mbaya sana nikahisi kama mtoto anataka kujifungua, ikabidi niikongoje hadi shambani kwa mama na nilipofika nikawa nimeangua pale shambani, mama akaja anakimbia na kuniokota, kisha akanipatia kikombe cha uji aliokwenda nao shambani. Ndipo nikapata nguvu kidogo mama akaamua kunikokota.
Mpenzi msomaji, usikose kesho kujua ni wapi mama Kecho alimkokota mwanaye kuelekea wapi?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U


      edit