Nimshukuru Mungu kwa
kunipa nafasi ya kukutana nayi kwa siku nyingine tena, karibuni katika
kujifunza kuhusu uhusiano katika maisha yetu ya kila siku.
Mada yangu ya leo
nitazungumzia watu ambao wanadhani wakitambulishwa basi inakuwa nikifungo kwa
mtu aliyemtambulisha kwa maana ya kuolewa au kuoa, wakati ukweli unaweza usiwe
hivyo.
Swala la wapenzi
kutambulishana katika familia za pande zote mbili kwa maana ya mwanamke na
mwanaume ni sehemu ya utamaduni wa jamii kubwa ya Kiafrika na ni jambo jema
sana. Ila kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza kwa baadhi ya wanaume na hata
wanawake, nianza na wanawake.
Unaweza ukapata mchumba
ambaye akapanga mipango yote kwa kuanza kukutambulisha kwa baadhi ya ndugu zake
ambao yeye anaivana nao au anaelewana nao sana na wewe mwanamke ukaona kama
umeishamkamata kwa kila kitu, kwani baadhi ya dada aua kaka zake wanakufahamu
na kukuita wifi au shemeji na wakati mwingine hata shangazi. Wakati huo
mwanaume mwingine anaweza kufanya taratibu zote za kuja kwenu kujitambulisha
kwa utambulisho feki ili kukuaminisha lakini mwisho wa siku akawa hana dhamila
ya dhati ya kutaka kukuoa zaidi ya kula tunda.
WANAUME
Mara nyingi baadhi ya
wanaume wengi wamekuwa wakilalamikiwa kuwa ni sehemu ya kuzalisha matatizo
yanayosababishwa na uhusiano.
Kuna watu wamewahi
kuumizwa vibaya kwa kutambulishwa na wapenzi wao lakini mwisho wa siku
wakaachwa solemba kama waswahili wasemavyo.
Mrembo mmoja aliwahi
kupata bwana na akaonesha msimamo mzuri wa kumwambia jamaa kama ana mpenda kwa
dhati na ana malengo naye kwa maana ya kuwa mke na mume basi wakatambulishane,
kijana alikubali wakapanga siku na muda wa kufanya huo utambulisho, siku
ilipowadia mwanadada akatambulishwa lakini mwisho wa siku aliyeolewa ni mtu mwingine.
Inaumiza na ilimuuma sana
binti yule kwanza ukiangalia umri wake alikuwa bado binti mdogo lakini hicho ndicho kilichotokea.
Kila mtu anapaswa kuwa na
hofu ya Mungu anapaswa pia amuonee huruma mwenziye ni kwa namna gani ataumia
pindi atakapomdanganya kuwa anamuoa aua kuolewa naye wakati moyoni mwaka anajua
kabisa kuwa hana mpango wa kumuoa.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U