NILIPOISHIA…
Huwezi kunitenganisha na familia yangu,
siwezi kuondoka kwenye nyumba ya bure nikapange, kama unalipa mwenyewe, twende,
pumbafu, kama hutaki, huwezi kuishi basi ondoka wewe,” akafunga vishikizo vya
shati lake kisha akaondoka.
ENDELEA NAYO…
Nilimuita, Maiko sina nia mbaya mpenzi wangu
nachotaka ni kuwa na amani, basi akarudi na kuniambia kwa hiyo una maanisha
mama yangu anakufanya unakosa amani, si ndiyo, yaani wewe mwanamke ungejejua
nilikupiga mimba kimakosa sana, sikujua kama ni kichwa maji hivi, huku ananikoa
kichwani.
Nikabaki nimejikunyata kwa kuhofia kipigo
zaidi, Maiko huyo sikumuona hadi baada ya siku mbili kupita, kila nilipomtafuta
kwenye simu, simu yake ilikuwa inaita bila majibu. Nililia sana kwa kweli,
kwani niliamini angekuwa msaada kwangu lakini ndiyo mtu anayeongezea
kushindilia msumari kwenye kidonda nilichonacho.
Muda mwingi nilikuwa nikishinda ndani mara
nilipokuwa nikimaliza shughuli zangu nilizopangiwa kimyakimya. Nilikuwa
nikitafakari sana juu ya maisha yangu na Maiko hasa kama tutaendelea kuwa
mikononi mwa wazazi wake, nilichokigundua ni kwama Maiko hajiamini kama
angeweza kupanga na ndiyo maana hakutaka kuhama kwao, kwa kuamini kuwa hawezi
kulala njaa wala kukosa nauli kutoka kwa mama yake ambaye alikuwa mpika
vitumbua maarufu mtaani kwao.
Sikuchoka kwamwambia ukweli na namna
ambavyo hatari kubwa nilikuwa naiona mbele yangu lakini siku zote hakunielewa
zaidi ya kunigeuzia mimi kibao, eti siwapendi ndugu zake, hata mama yake
nimekuwa nikimdharau. Muda mwingi nashinda nimejifungia ndani badala ya
kumsaidia mama kazi mbalimbali.
Baada ya miezi kadhaa kupita nikagundua
kuwa mguu mtoto wangu wa kulia ulikuwa umepinda ni kama mlemavu, yaani unyanyo
umegeuka pembeni, hata akikuwa hawezi kutembea kama mtu mwingine ambaye ni
mzima.
Je
nini kilifuatia, baada ya kugundua mtoto wake ana mguu umejikunja. Usikose
kesho kuanzia saa 9 mchana.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au
0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U