Wednesday, January 18, 2017

Published 1/18/2017 02:00:00 PM by

KUIONA PEPO BILA KUFA NI NGUMU!

Hivi kwa nini watu wengi hawapendi kujipanga na kuzungumzia kifo, namna ambavyo siku akiwa amefariki dunia, namna ambavyo ndugu, jamaa, marafiki na watoto wako watahangaika kwa sababu hukuwatengenezea mazingira mazuri.
Mateso watakayoyapata watoto wako kama ndugu, jamaa zako hawatawathamini. Namna ambavyo mtoto au watoto wako watashindwa kuendelea na shule ya private na kuamishiwa shule za Kayumba.
Hivi ujiulizi ni namna gani watoto wako watakavyolala njaa wakati pengine ulitafuta kwa ajili yako. Umewahi kufikiria vile umati wa watu wamezunguka jeneza lako kwa ajili la kuaga mwili wako. Mama, baba, watoto, mkeo au mmeo anavyolia kwa huzuni kwa kuwa hatokuona tena. 

Kaka, wadogo zako wanavyogaaga kwa sababu msaada wao umeondoka huku baadhi ya ndugu na jamaa wakifurahia kifo chako kwa sababu tu wanadai ulikuwa ni mtu wa kujiona, kujisikia na kujidai au ulichukua wake  au waume zao, uliwasumbua vijana au mabinti zao.
Pata picha sasa mwili wako unasafirishwa kutoka kwenye jumba lako la kifahari na kupelekwa sehemu ambayo ni kijiji kwenu na kwenda kusitiliwa kwenye shamba la ukoo. Uliowapenda wakaondoka nakukuacha peke yako ukiwa umefunikwa na tani za kutosha za mchanga.

Jaribu kufikiria ni maisha yapi ambayo utakuwa nayo huko chini ya aridhi wakati ukiwa pekee yako, jamaa uliokula nao bia, nyama, na kushea nao mapenzi hawapo tena. Kwa sababu tu zamu yako ikifika unaondoka pekee yako.

ITAENDELEA…

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U

      edit