NILIPOISHIA…
Niliamua kurudi nyumbani huku nikiwa nalia
njia nzima, niliona kama nimejiabisha sana pale kijijini na kuwaabisha wazazi
wangu. Mbaya zaidi kuna vijana ambao walikuwa wananitaka lakini niliwakataa kwa
sababu tu ya Maiko.
SONGA NAMI….
Niliendelea na maisha kama kawaida ila
akilini mwangu nilikuwa na michubuko mikubwa na mingi sana ya mapenzi
iliyosababishwa na mwanaume niliyempenda, moyoni nako nilikuwa nimejeruhika
mno, mkidonda ambacho naamini siwezi kumpata tabibu wake, kiasi kwamba sikuwa
natamani kupenda au kukutana na mwanaume ambaye ataniambia kuhusu habari ya
mapenzi.
Kwa kifupi nilikuwa nasikia tu watu
wakisema kuwa Fulani kaathirika kisaikolojia, sikujua maana ya kuathirika huko
ila kwa kipindi hiki nilicho nacho ndiyo haswa nimegundua maumivu ya mapenzi na
kuathirika huko kisaikolojia.
Kumbe wanaume ndivyo walivyo, wanapenda
kutumia na kukimbia, ni kwa nini wanafanya hivyo? Je, anakuwa hajakupenda, kama
ndiyo kwa nini anakubali kuduu na wewe? Au nilifanya vibaya kumwamini na
kumkabidhi moyo wangu.
Niliendela kujiuliza nikiwa nimekaa
pembeni ya mafiga nikisuri chungu cha ugali kiendelee ‘kupogoma’.
Nimeumia sana, moyoni mwangu kwa kile
ulichonifanyia Maiko kama ulikuwa huna mpango na mimi usingenilaghai hadi kuja
nyumbani kwetu na kuniaminisha kuwa uko tayari kuwa na mimi katika maisha yako.
Sura yangu nitaiweka wapi kwa wanakijiji
mimi, wamenisema sana kuwa napenda wanaume wa mjini wenye pesa, vijana nao
wamenidhihaki sana kwa wewe Maiko kunitumia na kunikimbia.
Wananiona sifai, kwa sasa hakuna hata
ambaye anataka kunitongoza kila mtu ananisonya na kuninyooshe kidole ‘shauria
yako utazeeka bila kuolewa, si unapenda wa mjini,” baadhi ya vijana wa kijijini
walikuwa wakiniambia hivyo.
Nilizidi kuumia kutokana na maneno ya
wanakijiji hasa wakiwemo wanaume ambao waliwahi kunitaka kimapenzi, mwili ulianza kudhoofika kwa
sababu ya mawazo, nikijiona kama mkosaji sana.
Baada
ya mwili kuanza kudhoofika nini kilifuatia.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea
www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U.