NILIPOISHIA…
Mama alinipa kikombe kimoja cha uji
aliokwenda nao shambani. Ndipo nikapata nguvu kidogo mama akaamua kunikokoa
kuelekea….
SONGA NAMI…
Basi kidogo nikawa na ahueni hata nguvu
kipata kidogo, mama alimua kunikongoja kuelekea hospitalini kwanu hakuwa na
pesa ya kuweza kulipia usafiri, kutoka kijijini kwetu hadi eneo la zahanati ni
kama shilingi elfu tano kwenda , kwa hiyo na kurudi elfu tano ukijumilisha watu
wawili ni shilingi elfu ishirini.
Mama hakuwa na pesa hiyo hata mimi pia
sikuwa na kitu kwani nilimtegemea Maiko lakini hakuwa na msaada wowote pamoja
na kumsumbua mara kwa mara.
Baba wa kambo naye hakuwa na msaada
wowote, mara nyingi alikuwa anakaa porini akifanya shughuli zake za kukata
mkaa, lakini hata pesa aliyokuwa akiipata ilikuwa haimfikii mama zaidi ya
kwenda kunywa pombe na kutembea na wanawake wa vilabuni.
Tulipita polini na sehemu zingine ambazo
zilitisha lakini hatukuwa na namna zaidi ya kukabiliana na kila kitu
tulichokutana nacho njiani, jua nalo lilikuwa kali sana, nilihisi kizunguzungu
mara kwa mara.
Nilipomwambia mama kuhusu kuhisi
kizunguzungu basi alitafuta mti wenye kivuli na kuniweka chini ili nipumzike,
hakina mwanamke maisha yake ni ya shida sana.
Tuliendelea na safari yetu baada ya kupiga
hatua kadhaa hali yangu ilianza kuwa mbay, nilianza kuhisi uchungu wa ajabu
ambao sijawahi kuuhisi katika maisha yangu, ni ngumu kuelezea maumivu ya
uchungu ule ulivyokuwa.
Nilianza kupiga kelele nikimuita mama
yangu, “mamaaaaaaa, mama.”
Je, kelele za msichana Kecho zilikuwa ni
za nini , na je watafanikiwa kufika kwenye zahanati ya kijiji na kujifungua
salama.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au
tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U