Mimi ni mdada wa miaka 26 nimejaliwa kupata mtoto
mmoja kwa mwanaume ambaye alinipa mimba na kunitelekeza, kwa kuwa nilikuwa nyumbani mateso hayakuwa
mengi zaidi kama nionavyo kwa wanawake wenzangu wengine.
Baada ya miaka
kadhaa nilikutana na mwanaume mwingine na kuanzisha naye uhusiano, jamaa
ananipenda na kunijali sana semas namuona kama siyo mwaminifu, muda mwingi yuko
bize na simu yake, na anapenda sana kuongea na wanawake. Nikimuuliza anasema
kuwa ni rafiki zake wa kawaida tu.
Roho inaniuma sana naona kama ananidanganya kabisa,
naomba ushauri wako, nifanyeje ili ajue maumivu yangu ninayoyapata?
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U