Habari yako,
Naitwa Mwana nini mdada wa miaka zaidi ya ishirini,
nilikuwa na mpenzi wangu ambaye ananizidi mwaka mmoja, na tumedumu kwenye
mahusiano kwa miaka miwili lakini ghafla Novemba mwaka jana akaniacha bila kosa
wala sababu zozote zile za msingi.
Nilijaribu kumuuliza kwa nini kachukua maamuzi hayo,
akasema kuwa ana mambo mengi sana ya kufanya hivyo hataki kujihusisha na
mahusiano ya aina yoyote ile.
Alinitumia ujumbe kuwa nimekuwa mwaminifu sana kwake,
hivyo hapendi kuja kuniumiza huko mbeleni, sijamuelewa maana ya maneno yake.
Ila juzi kati nilialikwa kwenye sherehe ya rafiki yake
kumbe na yeye alialikwa ila alikuja na msichana ambaye inaonekana kabisa ni kama
mpenzi wake, naumia sana napomuona kwa sababu naishi mtaa mmoja na huyo mpenzi
wangu.
Kumpenda bado nampenda sana, je, nawezaje kuepukana na
haya mateso mwenzenu?.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U