Monday, January 16, 2017

Published 1/16/2017 06:00:00 PM by

ZIJUE SABABU ZA KUACHWA NA KILA MPENZI!-2

Karibu katika muendelezo wa mada yetu ya jana inayozungumnzia sababu za kuachwa na kina mpenzi unayempata katikia maisha yako.
Jana nilitaja sababu moja wapo kuwa inawezekana nyota zenu zikawa haziendani, hazishabihiani na ndiyo maana mapenzi au ndoa yenu imejaa mikosi, imejaa malumbano, imejaa mifarakano ya mara kwa mara.
 Kitu cha pili kinachoweza kukufanya ukawa unaachika au unaachwa na kila mpenzi unayempata ni:


UNA MASHETANI
Kuna wengine inakuwa kama wana mashetani unaweza kukuta mtu kampata mpenzi ambaye ni mstaarabu lakini yeye sasa akawa aeleweki mara vile mara hivi kiasi kwamba kila mtu anakushangaa Labda Una Mashetani Au Umerongwa? 

Pamoja na vitabu vya dini kufahamu kuwepo kwa uchawi na ushirikina lakini binafsi sipendi ulipe nafasi sana suala hili na kama inapotokea kuwa hicho kinachosemwa au kuhisiwa ni kweli kimekukuta  basi mshirikishe Mwenyezi Mungu katika kukutatulia jambo hilo maana hashindwi hayo mashetani/ maurogo yako yatakwisha tu.

MAJIVUNO


Wengine huachwa na wapenzi wako kwa sababu ya majivuno kutokana na kitu flani ambacho anacho, unakuta ukikaa mbele za watu ‘full’ kujitapa, mara una cheni za gold, mara una gari zuri, unakula, kulala na kuvaa vizuri na majivuno mengine kama hayo kana kwamba hutokufa.

yawezekana kweli hivyo vitu unavyo kweli ila unavyogeuza vitu hivyo kuwa majigambo unamkera mwenzio kama yeye hana tabia kama yako kwani inafika sehemu unajivuna mbele ya ndugu, jamaa na hata marafiki zake, yaani inakuwa kiama unamtenganisha na jamii yake.

majigambo yako kila mnapokwazana na mwenzio unamsimang'ia ndugu zake, matusi na kejeli za hapa na pale kama ni mwanamke ni kutafuta doti za kanga kwa kwenda mbele, shauri yako utaishia kununu doti za kanga jamaa anakukimbia.

Hili la majnivuno ni la kuepuka pia katika mahusiano yako, kwani hata Vitabu Vitakatifu vinakatqaza majivuno.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U
      edit