Wapenzi
wasomaji wa ujasiriamali karibu kwenye
mada nyingine ya namna ya kufanya
biashara kwa njia ya mtandao.
Kila
siku dunia inazidi kutanuka na wanadamu wanazidi kubuni na kugundua vitu vingi
zaidi kwa ajili ya kurahisisha maisha ya kila siku.
Leo
nitazungumza nanyi kuhusu kufanya biashara kwa njia ya mtandao.
Biashara ya Mtandao ni njia ya kisasa ya
usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani hadi kumfikia mteja au mtumiaji moja kwa
moja, sehemu yoyote alipo.
Biashara
hii inazidi kujizolea umaarufu sana, kwani ni rahisi, nyepesi katika kuitangaza
pamoja na kuwafikia wateja mapema na haraka zaidi popote walipo duniani.
Unaweza kuuza, kununua bidhaa, kutoa au kupokea
huduma kutoka kwa watu au kuwapa bidha wateja wako kwa kupitia biashara hii.
Baadhi
ya watu wanaofanya biashara hiyo ya mtandao kwa kupost matangazo, kwa Tanzania
ni pamoja na Wema Sepetu, Mirad Ayo na wengine, kutoka nje watu maarufu duniani wanaoamini
katika biashara hii, yuko Robert Kiyosaki (Mwandishi wa vitabu vya Rich dad poor dad) rais
wa zamani wa marekani, Bill Clinton aliyewahi kuyashukuru baadhi ya makampuni
ya Network Marketing katika hotuba yake kwa kuwapa watu fursa sawa na
kubadilisha maisha yao. Lakini pia Bill Gates, aliwahi kuulizwa kama
angefilisiwa na kuanza upya angefanyeje?. Yeye alisema tu kwamba angechagua
biashara ya mtandao.
WAPO
watu hawana majina kama mastaa ila wana majina kwenye mitandao kwasababu ya
biashara zao za mitandaoni huku kukiwa na makampuni zaidi
ya 5,000 yanayofanya biashara ya mtandao duniani.
Watanzania
ifike sehemu tuachane na zama zile za kupiga picha za ajabu na kuziweka
mitandaoni, tubadilike tuitumie mitandao hii kibiashara zaidi, sio kutukanana,
kulumbana na kuanzisha mada zisizo na faida kwa jamii yetu.
Tukutane sehemu ya pili ya
mada hii.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745 au 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U