KAMA
ulikuwa haujui, basi hujachelewa anza sasa kufikiria kuhusu matatizo au
changamoto zinazopatikana maeneo mbalimbali yanayokuzunguka na kweingineko,
kisha fikiria kuyageuza matatizo hayo kuwa fursa kwako kutengeneza pesa
lakini pia kuisaidia jamii husika.
Wagunduzi
wa Mitandao ya Kijamii kama Facebook, tweeter na mingineyo walibaini uwepo wa
tatizo la watu kushindwa kuwasiliana na kupata taarifa kwa njia rahisi na ya
haraka, ndiyo maana wakafikiria kuanzisha huduma hizo ili kuweza kurahisisha
mawasiliano lakini kumbe kugundua urahisi huo kukawa ni faida kubwa kwao kwani
kuna watu ambao wanashika nafasi za juu duniani kwa utajiri walio nao ugunduzi
wa mitandao hiyo.
Maisha
yetu sehemu kubwa inazungukwa au kuendeshwa na matatizo mbalimbali, yawezekana
matatizo ya kipato kwa maana ya ajira, njaa, elimu, tiba, maji, huduma na
kadhalika.
Kikubwa
cha kujifunza hapa ni kuangalia nini unaweza kukitatua baadhi ya matatizo
unayokutana nayo au unayoyafahamu.
Ngoja
nikupe mfano, kutokana na kuhangaika kila siku kutafuta chakula huku na kule
kwenye vibanda vya mama lishe kuna siku nikiwa nimejilaza kitandani niliwaza.
Je, ni watu wangapi wanahitaji huduma ya kupata chakula kwa haraka tena wakiwa
wako maeneo yao ya kazini, ofisini, shambani, shuleni, na kwengineko? Nilifikiri
kwa muda kisha nikapata jibu la kuwa kuna kila namna ya kuanzisha
mchakato wa kutoa huduma kwa watu walio mabachela, walioko makazini au
wasioweza kupata nafasi ya kwenda kutafuta chakula kutokana na mazingira ya
kazini au maeneo wanayoishi.
Hilo
lilikuwa ni wazo langu mara baada ya kuhangaika sana kila muda wa kupata
chakula unapofika, na hilo linachangiwa na mazingira ya eneo ninaloishi. Hivyo
basi jaribu kuchunguza na wewe kisha iwe akili yako muda wa kufikiri kile
ulichokibaini kisha tafuta jibu lake (unaweza kunishirikisha kwa
kuniinbox) ni changamoto zipi ambazo unakutana nazo kila siku kiasi kwamba
umekuwa ukitamani apatikane mtu fulani wa kuzitatua, lakini kabla ya kufikiria
kupata mtu wa kuzitatua changamoto hizo.
Kwa nini mtu huyo usiwe wewe?
Kwani
huyo unayemfikiria yeye ameumbwa kwa kivipi na wewe umeumbwaje? Kama yeye
ataweza kwa nini wewe usiweze?
FUNGUKA
WIGA WAKO NDIYO UMASKINI WAKO. Usiogope kupata hasara ni sehemu ya changamoto
pia ambazo zitakukomaza na kukufikisha unapopataka.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U