NILIPOISHIA….
“Lakini ndiyo tayari nimeishaliwa, sina
namna, nihesabu fungu la kukosa nikaanze maisha mapya kuliko kuendelea
kuteseka, kama wameweza kumtafutia mke mtoto wao watashindwa kweli kunipa sumu
kwa sababu namng’angania mtoto wao. Kama ni umaskini nimezaliwa nao, acha
niendelee kuwa nao tu,”nilizidi kuwaza kichwani.
“Samahani dada eti stendi ya kwenda mjini
iko sehemu gani?”
ENDELEA…
“Nyoosha hivi kulia, kisha kata kushoto
endelea tu hadi upite mti mkubwa alafu kata tena kulia utaiona kwa mbele yake
kidogo.” Alinijibu Yule dada.
Nilikuwa nimechoka sana kwani njia
sikuifahamu sana, sikuwa na uwezo wa kukodi pikipiki kwani hata nauli ambayo
nilikuwa nayo nilijaribu kudunduliza nilipokuwa naachiwa matumizi. Yaani efu
saba niliyokuwa nayo niliamini kama nitaigusa basi nitaishia kuwa nazunguka tu
Morogoro, hivyo nilijitahidi kutembea hadim hadi nilipofika stendi. Nilipata
gari, nikaingia na kumuhamishia mtoto wangu kifuani kisha nikaka ili kusubiri
muda wa kuondoka, nilipitiwa usingizi mzito, uliochanganyikana na njaa pamoja
na mawazo chungu mzima.
“Mwanangu jitahidi sana kuvumiliana na mwenzako,
hata mimi hapa kwa baba yako siyo kwamba namaisha ya raha, wewe mwenyewe unaona
kabisa wakati mwingine hatuli, wakati mwingine anakuja kalewa na kuanza kufanya
fujo.
“Lakini nimevumilia mwanangu kwa tabu
hivyohivyo pamoja na msimango kuwa wewe ni mke wa mtu anakuhangaikia kukulisha,
katulie mwanangu, manyanyaso, matusi mama vumilia kwa sababu baba yako huwa
hataki kukuona kwake na kama utarudi basi ujue mama yako nimeachika, sasa
mwanangu kwa umri huu niachike nitaenda wapi mimi, nani atanioa.” Niliendelea
kuwaza zaidi.
“Kama ndivyo nitaenda wapi sasa jamani,
kwa maneno yale ya mama sitakiwa kurudi kule kijijini na kama nikirudi basi
nirudi kuivunja ndoa ya mama yangu, kwa uzee ule ataenda wapi mskini mama
yangu, nani atamuomba mama yangu?” Nilibaki nikijiuliza mwenye maswali
mengimengi kichwani mwangu, machozi yakaanza kunitoka, na kujilaumu kwa
kumuamini Maiko.”
Lakini wakati mwingine nilimuona Maiko ni
kama hana makosa, labda pengine anazidiwa nguvu na familia yake, ila namlaumu
kwa kuwa mwanaume suruali kwa sababu moja, ni mwanaume gani wa miaka zaidi ya
ishirini na tano unashindwa kujitegemea!? Unashindwa kuwa na maamuzi yako
binafsi kuhusu maisha yako!? Unakuwa mwoga na maisha, kama mwanaume unakuwa
mwoga kiasi hicho vipi kuhusu dada zako!? Hii ni hatari na madhaifu makubwa
sana kwa Maiko.
Kecho
anazidi kujiuliza sana kichwani mwake kuhusu maisha yake, kuhusu tabia ya woga
aliyonayo mzazi mwenzake. Je, nini kilifuatia?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U