Mimi ni msichana wa miaka 23, nina mpenzi wangu ana
miaka 28 , tuko kwenye mahusiano kwa mwaka sasa.
Sehemu.ninayofanyia kazi kuna baada sasa kuna siku
kulikuwa na sherehe ingawa siyo mlevi ila siku hiyo nilikunywa sana hadi
nikalewa nikaenda kwake nikiwa nimelewa.
Alikasilika sana kwa mimi kulewa ila akanisamehe,
maisha yakasonga kuna siku nyingine nilimpigia simu na kuuliza yuko wapi
akasema anatoka kupokea watoto shule. Nilimuuliza wa nani akasema kwa kwake,
nilishangaa sana na kumwambia mbona hakuwahi kuniambia kama ana mke au watoto.
Akasema ndiyo amewaleta niwalee, nilipaniki nikamwambia anakichaa na siko
tayari niwalee watoto wa mwanamke ambaye simjui.
Akakasirika sana na kusema hawezi kunisamehe,
nimemuomba samahani mara nyingi kwenye simu anasema atanisamehe, nikaongea na
dada zake wananifahamu akawaambie kuwa niende nyumbani atanisamehe.
Muda umepita bila kumsamehe, naumia sana kwani.bado
nampenda.
Nilienda kwake sikumkuta ila mmoja wa majirani
alinivuta chemba akaniambia mpenzi wangu kuna siku alikuja na mwanamke ambaye
ni rafiko yangu niliwahi kwenda naye.kwa mpenzi wangu ili akanisaidie kuomba
msamaha.
Yule rafiki yangu inasemekana alilala pale hadi
asubuhi, nilimwambia mpenzi wangu kuwa amenisaliti kwa kutembea na mpenzi wangu
lakini nimemsamehe naomba turudiane akasema hanipendi. Naomba ushauri wako
nifanyeje na mimi nampenda sana.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745 au 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U