NILIPOISHIA
…
Nilifikiria sana juu ya maisha ya mwanamke
na kugundua kuwa sehemu kubwa ya maisha ya mwanamke ni kama yamejaa mateso zaidi
kuliko furaha, kwani kupata mwanaume mkweli na mwenye mapenzi ya dhati ni mara
chache na ni bahati kubwa, kama kupata kwa jua kule kullikotokea mkoani Mbeya
ENDELEA
NAMI…
“Hivi ni kwa nini wanaume hawawaonei
huruma wanawake kuacha kuwaumiza, matokeo yake kila siku wanawaumiza, wanaume
ni watu wa aina gani wasiyokuwa na chembechembe za upendo wa dhati kwa wapenzi,
wachumba au wake zao.
“Mtu kakubebea mimba yako miezi 9
anahangaika nayo, hivi ungepewa wewe ubebe kwa wiki moja, ungetamanika,
mwenziyo kabemba ujauzito alafu mwanaume mwingine yeye anaendelea kula bata,
anagawa vinjwaji tu baa. Kama nimchepukaji basi kapata nafasi, au kupombeka
kama ni mtu wa kilaji. Dah! Haya bana siniliamua kuishi na mume wangu acha
nivumilie.” Nilijikuta nikijisemea kwa sauti ya juu, sijui kama watu niliokuwa
nao karibu walisikia au la.
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo
ambavyo mawifi na mama mkwe wakazidi kujenga chuki juu yangu, hata mtoto wangu,
damu ya ndugu yao wakwa wanaisusia, yani kama nikienda kujisaidia mtoto akianza
kulia hakuna anayehangaika kumbembeleza hata kama yuko jirani au anapita jirani
naye. Nilizidi kujihisi vibaya sana, kwani nini inakuwa hivi , mbona mimi nina
uhakika hii ni damu ya Maiko, au wao wamepata wapi uhakiki kuwa Gift siyo damu
yao.
Ikafika kipindi hata salamu zao nikawa
sizipati kama zamani, nilikabaki kuwa mtu wa kulia tu kila siku, kila mara,
maana wakati mwingine wananifanyia kusudi tu ilimradi nisiimalize siku kwa
amani, ama kweli kuna watu wanafigisufigisu duniani. Sikuwa na namna kwa sababu
niliamini nampenda sana Maiko wangu, na sikuwa tayari kutenganishwa naye, hivyo
nilijiapiza kupigana na changamoto zote ninazokutana nazo.
Lakini kuna wakati nilihisi kukata tamaa
kwa sababu mtu ambaye nilimtegemea kama msaada kwangu, kumbe hakuwa upande
wangu, alikuwa kwenye familia yake, kwa hiyo ikawa ni mimi, Kecho dhidi ya
Familia ya Maiko. Asikwambie mtu ninataka moyo, sana lasivyo unaweza kuchukua
maamuzi magumu.
“Maiko
mpenzi wangu wangu mimi nimechoka na maneno ya ndugu zako, kweli kila siku
mpenzi wangu, mimi tu ndiyo nitakuwa mkorofi?” Nilimuhoji
Unajua
nini alichomjibu maiko, usikose kesho muda kama huu.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U