Sunday, January 22, 2017

Published 1/22/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-17



NILIPOISHIA…
“Maiko mpenzi wangu wangu mimi nimechoka na maneno ya ndugu zako, kweli kila siku mpenzi wangu, mimi tu ndiyo nitakuwa mkorofi?” Nilimuhoji.

SONGA NAMI…
“Wewe hujijui, si ndiyo,”
“Halafu naomba ukome kumsingizia mama yangu kama umeshindwa kukaa hapa na mama , basi wewe rudi kwenu.” Hayo ndiyo majibu ya Mume wangu.

Nilijaribu kila kila aina ya njia ili kuwe na amani, lakini ilishindikana, nikazidi kuchokana sana, kwani siku kuimaliza pale nyumbani ilikuwa ni kama mwaka, tena mwaka wenye mateso, yaani, mvua, jua vyako, sijuii, kuumwa, kuuguliwa, kufiwa vyote vyako.

Nilijaribu kujifanya mpole na mnyenyekevu kwa Maiko kwa wiki nzima, nikimpetipeti kwa kila aina, kila alipotoka kazini nilimpokea kwa kumuwao bila kujali ndugu zake watasemaje, lengo langu lilikuwa ni kumuweka karibu zaidi Maiko ili siku moja abadilike kifkra na achukue maamuzi yenye busara ili tuweze kwenda sehemu nyingine kuanza maisha nje ya nyumbani kwao.

Kuna siku nilijifanya kuchukua maamuzi magumu na kumwambia kuwa tuhame pale nyumbani kwao, kama hawezi kuhama basi mimi nimwache na mtoto wake, akaseme niondoke hata muda ule ila niondoke na mtoto wangu. 

Nikanyanyuka kitandani, nikamsogelea Maiko na kuingiza mkono wangu kwenye mkono wake aliokuwa amejishika kiunoni, nikamwambia kwa sauti ya upole na yenye mahaba, “Maiko kipenzi change, nakupenda sana lakini hapa kwenu si sawa kuendelea kuishi, wewe ni mtu mzima sasa, una familia, unatakiwa na wewe kuwa na kwako, haiwezekani baby kwa umri huu bado uwe unategema chakula cha kengele, ni heri tukalale njaa ila tuko kwetu.”
 
Nikasukumwa, nakwambia, “ni kwa nini wewe mwanamke unataka kunipanda kichwani, au umeishapata vibwana bwana uchwara huko mtaani na ndiyo vinakupa kiburi, si ndiyo. “Huwezi kunitenganisha na familia yangu, siwezi kuondoka kwenye nyumba ya bure nikapange, kama unalipa mwenyewe, twende, pumbafu, kama hutaki, huwezi kuishi basi ondoka wewe,” akafunga vishikizo vya shati lake kisha akaondoka.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
      edit