NILIPOISHIA…
Nilimchukia sana baba wa kambo moyoni mwangu, sikujua
kama mimi nimekuwa mateso na msimango kwa mama yangu, nilianza kumfikiria Maiko
na kuona kumbe wanaume wote ni makatili sana, basi nilimuahidi mama kuwa niko
tayari kwenda
ENDELEA…
Pamoja na kumchukia baba wa kambo niliamua kumuaga ili
asije akapata kisingizo kingine. Nikachukua kimfuko change pamoja na kimkoba
cha kiaina na mwangu, nikamuweka begani safari ikaanza, nilichukua usafiri wa
baiskeli hadi mjini kisha nikaelekea stendi, nilichukua gari la kwenda
Morogoro.
Niliwa safarini niliendelea sana kuwaza juu ya maisha
ya mama yangu, kwani niliona ni mwanamke ambaye anapitia mateso sana ingawa na
mimi niliyapitia lakini kitendo cha Maiko kunitumia nauli na kuniita kwao
kilinipa tumaini jipya katika maisha yangu, niliona ni muda mzuri wa kwenda
kuishi na mzazi mwenzangu huku nikiwa nashauku
kubwa ya kumsaidia mama yangu awe na kitu cha kushika hata kama
atendelea kuwa na mume wake.
Niliona tumiani jipya kabisa katika maisha yangu ya
mapenzi, kwani Maiko ni mwanaume ambaye nilikuwa nampenda sana na sikuwahi
kuwaza kumsaliti hata siku moja, hata kama atakuwa amenikosea kitu
gani.Nilihisi maisha yangu bila Maiko si chochote wala lolote, kwa jinsi
nilivyompenda.
Akili yangu ilihama kabisa kwenye gari na kujikuta
ikihamia kwa Maiko, nikifikiria ni kwa namna gani tutakavyoishi maisha yetu
mimi na yeye. Nikiwa nimezama katika dimbwi zito la mahaba na mwazo juu ya
maisha mpya, hatimaye gari linatia nganga katika Stendi Kuu ya Msavu, Mjini
Morogoro.
Kwa mbali namuona Maiko akiwa anakuja kwa mwendo wa
shauku na kunikumbatia kisha anamchukua mtoto na kumbeba, anamfunua na
kumuangalia.
Maiko akanipa hongera kwa kujifungua salama, kiukweli
ni kama alinitonesha kidonda changu ila kwa kuwa alikuwa ameomba msamaha na
kunitaka tukaishi naye wote sikuwa na nafasi ya kuyapa nafasi yale maumivu ya
awali.
Nini kilifuatia usikose kesho, Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U