Monday, January 30, 2017

Published 1/30/2017 02:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-24




NILIPOISHIA…
Nashukuru Minza kwa uji, kidogo angalau naweza hata kuongea, mwanzoni nilikuwa naona kama na wewe unaning’onga tu, mimi na njaa na uchovu afu wewe unataka umbeya tu.
Kwanza shoga yangu naomba nipumzike hapa kwako kwa siku kadhaa wakati najipanga kwenda kijijini kwetu, si unajua palivyombali na hata mia yenyewe sina

ENDELEA NAO…
Minza alinikubalia kwa sababu ni rafiki yangu wa muda mrefu sana , nilimsimulia mwanzo-mwisho kuanzia nilivyokutana na Maiko, nilivyoanza kufanya naye mapenzi, nikapata ujauzito, akapotea masikioni na machoni mwangu, nilivyotesekana na mimba yangu porini na hatimaye nikajifungua salama. Hadi leo hii Minza rafiki yangu unavyoniona hivi nimekonda ni kwa sababu ya hayo mambo niliyokutana nayo.

Minza lisikitika sana, akamlaumu sana Maiko na fam ilia yake, akwalaumu sana wanaume wote kwa kusema ni kama wanyama wakali wanaoharibu maisha ya wanawake wengi katika uso wa dunia hii.
Pamoja na Minza kunikubalia kwa kunipa hifadhi pale geto kwake ishu kubwa ilikuwa ni chakula, kwani hata yeye mwenyewe maisjha yake yalikuwa ni ya kubangaizabangaiza kwa kusukasuka.
 
Ingawa hilo la kuchangia pesa la chakula kwangu ulikuwa ni mtihani mwingine lakini niliona ni angalau kidogo kwa sababu nimepumua kutoka kwenye mdomo wa samba wenye njaa kali.
Basi nikawa nimefungua ukurasa upya wa maisha yangu, nikiwa pale Kibaha kwa Mfipa, ambapo ni kama cente au mjini mwa kijiji ninachoishi, kwa maana mtu akisema anataka kwenda mjini basi anakuja kwa Mfipa.

Baada ya muda niliwasiliana na mama na kumuomba aje mjini na nimuelezee lakini ishu ikawa ni nauli atapata wapi na kwa kipindi hicho mumewe alikuwepo, sidhani kama atampa nafasi. Hivyo niliendelea kukaa pale kwa muda mrefu bila kuonana na mama yangu wala yeye mama kuja mjini kwa sababu tu muda mwingi mumewe alikuwa nyumbani, hivyo ilikuwa ni ngumu sana kumuaga na kumruhusu.

Mpenzi msomaji Kecho kapata hifadhi ya kukaa kwa rafiki yake, kawasiliana na mma yake mzazi na kumsimulia kila kitu. Usikose kufahamu nili kilifuatia.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na:M&U
      edit