NILIPOISHIA….
Kwa kipigo kile mawifi na mama mkwe
walionekana kufurahia sana na wakati mwingine nilkikuwa nawasikia wakisema
watahakikisha hadi naondoka eti sifai kuwa mke wa kaka au mtoto wao, kwa
uanamke gani nilionao.
ENDELEA…
Hakika maisha yana mitihani sana, hasa
kwetu sisi wanawake, kila siku ni watu wa maumivu tu, nililia sana, muda mwingi
nikawa naishi kwa uwoga, sina amani, sina furaha yoyote ile moyoni mwangu,
nikaanza kuiwaza angalau kidogo amani ya kijijini kwetu kwa sababu pengine
aliyeteseka kana ninavyoteseka mimi ni mama yangu ila mimi nilikuwa na amani.
Ilifikia wakati mume wangu Maiko akawa
akienda kazini leo anarudi baada ya siku tatu, nikitaka kumuuliza anasema
nisimpangie wala kumfuatilia, nilipojaribu kuwashirikisha wazazi wake
sikuambulia kitu ni kama wanamuogopa Maiko au walidhamilia kunifanyia unyama
huo. Na nilipozidisha kutaka kufahamu basi niliamulia kipigo hasa, maisha yangu
yakawa ni ya kutukanwa, kukejeliwa na kipigo.
Sitaki kukumbuka siku ambayo
nilimnyenyekea mama mke na kumuomba anisamehe kama nimemkosea lakini hakunielew
zaidi ya kunitambia, “mwinga aache kuwa Mwasi ukawe wewe, usiye na mbele wala
nyumba, mwanamke gani hutingishiki, nyumba na mbele hakueleweki, umekuza nido
tu.
“Ebu nyanyuka hapa usiniachie laana bure
mtoto wa mwanamke mwenziyo,”mama mkwe alinisukuma na kuondoka huku nyumba watoto
wake wa kike ambao ni mawifi zangu wakianza kucheka.
“Mijitu mingine bhan, utatolewa jicho,
wewe fungasha urudi kwenu hapa huna chako, kaka Maiko leo anakuja na mwanamke
wake.” Kabla hata sijajinyanyuka mama mkwe alinirudia akiwa kafula kwa hasira.
“Hivi wewe Malaya kwa nini hujiongezi, visa
vyote hutaki kujiongeza si ndiyo, basi fungasha vilago vyako na kikaragosi
chako haraka sana uondoke hapa, tumekuchoka.”
Mawifi waliingia ndani na kunikusanyia
kila kilichokuwa changu na kunitupia nje, nililia sana. Wakaanza kunisukuma
huku wakiniambia nikamchukue na kidudu washa wangu (mwanangu Gift). Nilishangaa
wifi mkubwa aliingia ndani ambapo mtoto alikuwa amelala akamuamsha na kumbeka
kisha kuja kunitupia.
Nini kilifuatia baada ya Kecho kutupia
mtoto wake?
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745 AU 0679979785.
Pia
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea
ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U