Tuesday, January 24, 2017

Published 1/24/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-19



ILIPOISHIA…
Maisha ya pale nyumbani nikaanza kuyaona ni ya shida saana pengine ni nafuu hata na masimango ya baba wa kambo kuliko kusimangwa na familia nzima, si mawifi, si mama mkwe hadi baba mkwe, inauma kiukweli.


SONGA NAMI…
Baada ya miezi kadhaa kupita nikagundua kuwa mguu mtoto wangu wa kulia ulikuwa umepinda ni kama mlemavu, yaani unyanyo umegeuka pembeni, hata akikuwa hawezi kutembea kama mtu mwingine ambaye ni mzima.

Nilimshirikisha Maiko katika hilo lakini hakuonekana kujali, alidai yeye yuko bize na maisha, hivyo mimi kama mama ndiyo ninawajibu wa kumwangalia mtoto. Niliumia sana moyoni mwangu kwani mtoto huyo sikumpata peke yangu bali nilishirikiana naye kwenye mapenzi na ndicho tulichovuna.


Niliendelea hivyohivyo kumsumbua kiasi cha kuonekjana kero kwake, baada ya kumsumbua kwa muda mrefu kuna siku akanipatia pesa kidogo, nikampeleka mtoto wangu hospitalini ila nikaambiwa kuwa kwa Morogoro huduma hiyo haipatikani hadi niende jijini Dar Es Salaam ndiko mwanangu anaweza kupata huduma nzuri zaidi.

Pamoja na kumshirikisha mwenzangu bado alionekana halichukulii uzito suala hilo la mguu wa mtoto kupinda, nilizidi kuumia sana. Nilifikiria sana juu ya mwanangu Gift anapopata mateso ukubwani kama mimi mama yake nitazembea kama afanyavyo baba yake.


Misukosuko haikuishia nyumbani kwao Maiko na mara nyingi mambo mengi yaliyokuwa yakitokea mimi ndiye niliyekuwa nasingiziwa kuwa nimeyafanya. Ikafika sehmu Maiko akawa akirudi ananipiga sana kwa madai kuwa nimemtukana au kumbishia mama mkwe, kipigo nilichokuwa nakipata kinapelekea kunivimbisha mwilini na hata rangi yangu inabadilika unakuta jicho au shavu jekundu, kwa sababu ya magumi niliyopigwa na Maiko. 

Kwa kipigo kile mawifi na mama mkwe walionekana kufurahia sana na wakati mwingine nilkikuwa nawasikia wakisema watahakikisha hadi naondoka eti sifai kuwa mke wa kaka au mtoto wao, kwa uanamke gani nilionao.

 Je, mama mkwe na wifi yake watafanikiwa kumtenganisha na Maiko?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 AU 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
      edit