Sunday, January 15, 2017

Published 1/15/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA!-10




NILIPOISHIA…..
Miezi mitatu ilipita bila mtoto kupewa jina, akaendelea kunisumbua sana ikiwa mtoto ni wa kulialia tu mara kuugua, nikaamua kwenda tena kule center kwa ajili ya kumtafuta Maiko kwenye simu.

SONGA NAMI……..
Muda ulipita mtoto akiendelea kunisumbua, huku mama ana majirani wakidai ilikuwa ni lazima baba yake mzazi ampe jina ndipo atakaponyamaza.

Niliumia sana kwa hali hiyo kwani sikuwa natamani kabisa kumuona Maiko maishani mwangu, nilitamani kama ingewezekana kumpa jina mtoto wake hata kwa njia ya simu au SMS basi ningeomba afanya hivyo lakini haikuwezekana.

Niliendelea kufikiria namna ya kukabiliana na hilo bila kufahamu, nikiwa nimechoka kabisa kufikiria namna ya kumpata Maiko ili aje ampe jina mwanaye nilishangaa kupokea ujumbe ambao ulikuwa ni wasamahani sana kuhusiana na kile kilichotokea dhidi yangu na Maiko.

Ndani ya bahasha ile kulikuwa na nauli pia ya kutoka kijijini hadi mjini, mjini hadi nyumbani kwa wazazi wake Maiko ambao walikuwa kuwa wanaishi wilayani Ifaraka Mkoa wa Morogoro.
 
Sikuwa na furaha kwa samahani na pesa ile aliyonitumia eti, kasikia nimejifungua hivyo anataka akamuone mtoto wake pamoja na kumpa jina, kweli Maiko ni mwanaume wa ajabu, katili sana, anajua ni kwa jinsi gani mimi nimeangaika na mtoto wangu kuanzia mimba hadi kujifungua, na mbaya zaidi nimejifungulia porini, hadi siku hiyo mtoto wangu hakuwa amepewa chanzo wala dawa ya aina yoyote ile kwa sababu sina nauli ya kwenda zahanati.

Nilimsimulia mama kila kitu kilichotokea  na uchungu nilionao kuhusu Maiko, mama akanisihi sana na kunishauri ni bora niende kwa mzazi mwenzangu kwani pengine amejirekebisha, matatizo ya kwenye mapenzi huwa yapo tu hata yeye ana mambo mengi yanayomsibu na mumewe sema mengine huwa haniambii kama mtoto.
Je, Kecho alikubaliana na ushauri wa mama yake kuwa aende Morogoro kwa mzazi mwenziye?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U


      edit