Naombeni ushauri wenu wadau wa M&U mimi ni
mwanachuo nilikutana na jamaa mmoja ambaye ni mwanachuo na kuanzisha mahusiano,
kwa sasa tuna miezi miwili katika mahusiano hayo.
Awali nilikuwa nasikia tu kuwa jamaa ana watoto wawili
ambao alizaa na wanawake wawili tofauti, nikashtuka sana na kujiuliza mbona
hakuniambia?
Niliamua kumuuliza akakubali kuwa ni kweli ana watoto
wawili na anaomba nimsamehe kwani hao aliozaa nao hawapendi ila ananipenda
mimi.
Juzi jamaa kaja kwangu na ndugu yake wakiniomba
msamaha, ndiyo najiuliza nimsamehe ili tuendeee naye au niachane naye na
nifanye maisha mengine?.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U