Ni nyumba mpya ambayo kijana Mustafa anaishi
maeneo ya Kijitonyama, anaishi ndani ya chumba kimoja ambacho kina muonekano
mzuri sana, nikikubwa, kina mwanga na hata mama mwenye nyumba hana makuu kama
wa mama wengine wanavyokuaga na kero kwa wapangaji wao.
Maisha ya Mustafa ya wastani kwani anafanya
kazi kwenye kampuni moja ambayo ni kubwa kwa wastani, kwa kawaida hapendi
kulala akiwa ameweka neti kwenye kitanda na hapendi kwa sababu tu anahisi kama
anakosa hewa ya vizuri na pia anahisi kama akiweka neti anakuwa kama anabanana
, hivyo aliamua kila siku iendayo kwa mungu ni lazima anunue dawa ya mbu wa
ajili ya kupuliza chumbani kwake kabla ya kwenda kazini aliendelea na hali hiyo
kwa muda, lakini cha ajabu akawa anaona kila siku mbu wanazunguka zunguka ndani
ya chumba chake.
Akakukmbuka kweli nje ya dirisha lake kuna sehemu
waya wa kuzuia mbu umechanika hivyo alijitahidi kuweka kuweka mabox ambayo
yatazuia mbu wasiingie lakini inavyoonekana ni kama wanapenya kwa mbali, kitu
kingine aichokigundua ni baadhi ya nyufa kwenye mlango wake.
“Hata kama nikinunua neti muda mwingi huwa
nautumia nje ya neti nikichapa kazi zangu bado tu kama mbu wapo wanaendelea
kuniuma,”alikuwa anajiuliza mwenyewe kichwani.
Alifikiria kwa muda kutoka na kumaliza kumeza
dozi ya malaria lakini ndani ya siku tatu anashituka akiwa na vijipele vya kung’atwa
na mbu kwenye mkono wake wa kuume, kila muda alikuwa akivitazama vijipele vile
na kujiuliza kama kweli nitashindwa kujikinga na malaria nitawezaje kufikia
ndoto zangu.
Baada ya kujiuliza kwa muda alibaini kuwa
anafanya uzembe mkubwa sana kwa kwa mujibu wa takwimu mbalimbali ugonjwa wa
malaria unaonekana kuuwa sana binadamu kuliko hata ugonjwa hatari wa ukimwi.
Huku tawimu zingine zikitakwimisha kuwa kila dakika kunatokea kifo au vifo
vitokanavyo na malaria.
“hivi kumbe nacheza na kifo mimi mwenyewe,
nawezaje kuwa mzembe kwa kushindwa kuziba au kununua wavu wa shilingi 6000 kwa
ajili ya kutengeneza dirisha ili mbu wasipite, hivi kweli nakuwa mzembe kiasi
hiki wa kwa kucheza na kifo kwa [pesa kidogo kiasi hicho, huu ni ujinga,
natakiwa nisifikirie au nisiuugue ugonjwa huu hatari wa malaria ila ugonjwa
wangu mkubwa uwe ni kuhakikisha natimiza ndoto zangu,” aliendelea kufikiria.
Tangu siku hiyo kijana Mustafa akawa
anawachukia sana mbu na hata kama akienda sehemu akaona mbu wanarandaranda basi
utasikia makofi ya kuuwa mbu hao, kwani anaamini mbu hao wanaweza kukatisha
ndoto zake kubwa mabazo zinaweza kuisaidia jamii yake na taifa kwa ujumla. Anza
sasa kuchukua hatua kwa kununua neti na hakikisha unapulizia dawa sehemu
unapolala ili kuzuia malaria. Kwa kufanya hivyo utakuwa na nafasi kubwa ya
kuweza kufikia ndoto zako.
Shusha neti kwanza kabla ya kulala kisha omba
Mola ndiyo ulalale. Usiku mwema.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U