Sina maana ya kuwanyanyapa wale wote ambao wanaumwa au
ni waathirika wa ugonjwa hatari wa ukimwi ambao ni tishio duniani, kutokana na
idadi kubwa ya walimwengu kuaga dunia kutokana na gonjwa hilo.
Maisha yangu yalikuwa ni magumu sana yaliyojaa uchovu
wa hali ya juu sana hasa nilipokuwa narudi nyumbani kutoka kazini nikiwa
nimechoka. Huku nikifikiria namna ya kuanza kuosha vyombo, kuchambua mchele,
kupika, kutoa vyombo kuosha na kadhalika.
Hivyo vitu vilinitesa sana, kingine ni kuhusu kufua
nguo zangu, kwani ilikuwa ikifika Jumapili naanza kujiuliza Jumatatu hadi
Ijumaa ninavaa nini?
Kwani muda wangu wa kufua ulikuwa mchache hata siku
ambayo ilikuwa ni ya mapumziko nilipenda kuitumia kupumzika kwa kulala au kufanya
kazi zangu kwenye computer.
Niliendelea na maisha
hayo kwa muda mrefu sana huku uchovu na masumbufu ninayoyapata
yakinihimiza kuoa. Nilikuwa mwoga sana hasa ninapowaona, ninapowasikia walio
kwenye ndoa wanavyopigana vikumbo, wanapigana, kutukanana na kukejeliana
niliumia sana kwani katika maisha yangu sipendi dharau.
Yote kwa yote umuhimu wa kuoa niliuona, na nilihisi ni
muda muafaka kwani maisha ndiyo yaliyonifanya niwaze kuwa na msaidizi. Hatimaye
nilijitutumua ka kuyavulia nguo maji, nikatafuta mwanamke ambaye niliona
ananifaa na kweli nilifanikiwa kumpata. Nilijitambulisha kwao na kwetu pia, maisha
yaliendelea kama kawaida.
Baada ya muda niliacha kazi ofisi niliyokuwa na
kuhamia kwenye magari makubwa ya kwenda nje ya nchi. Sehemu kubwa ya maisha
yangu yalikuwa safarini kwani nyumbani.nilikaa mara moja au mara tatu kwa mwezi
au nisikae kabisa.
Kuna wakati nilikuwa nikienda nje ya nchi nakaa kule
kwa muda wa miezi mitatu bila kurudi nyumbani kwangu, mara nyingi nilikuwa
ninaunga hukohuko labda nimeenda Malawi, napitia Zimbabwe, Angola, Zambia kisha
Tanzania.
Kutokana na kusafiri sana ikafika sehemu mke wangu
akawa hana imani na mimi kila nikitoka safari alilazimisha twende kwanza
tukapime ndiyo anipe mchezo, hata kama nilifika usiku wa manane sikuweza kupata
lamabalamba hadi kunapokucha kisha ananipeleka hospitali kwa ajili ya vipimo.
Majibu yanapotoka basi nakabidhiwa mzinga wa asali najilia.
Nilizoea na hali hiyo ingawa kiukweli safarini kote
nilikuwa makini sana kwani nilikuwa naipenda familia hasa mke wangu. Baada ya
zoezi hilo kuendelea ikatokea siku moja nikarudi usiku afu ninaukame vibaya
nilipoomba kiaina kama kujaribu msimamo wa mke wangu ulikuwa ni ule ule. Tena
kuna wakati alinijibu kwa jazba kwamba kwa nini najifanya kujisahaulisha wakati
utaratibu naufahamu.
Nikawa mpole hadi kukachwa, tukaelekea hospitalini kwa
ajili ya kupima. Mungu huyu jamani, majibu yangu yalikuja nikiwa sijaambukizwa
Virusi vya Ukimwi lakini cha ajabu mke wangu kipenzi akakutwa ni mwathirika.
Nilitaharuki sana kwani yeye alihisi kuwa mimi
nikisafiri naenda kufanya uzinzi lakini yeyw ninayemuacha nyumbani kumbe
anachepuka. Niliishiwa nguvu nikabaki namuangalia mke wangu kwa jicho la
huruma, natamani nimrukie lakini nguvu sina, natamani nimtukane lakini maneno
hayatoki.
Nilifikiria sana jinsi jana yake usiku nilivyokuwa na
ukame alafu nikawa kama nataka kutumia nguvu kufanya naye tendo la ndoa. Sitaki
kuamini nimenuthurulika kwenye shimo la simba. Nimebaki njia panda panda, je
nimfukuze au nimfanyeje,. Vipi kama ungekuwa ni wewe ungefanyaje?
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U