Tuesday, January 3, 2017

Published 1/03/2017 03:00:00 PM by

FANYA HIVI MWAKA 2017 KUFIKIA MALENGO YAKO-3






Kwa mwaka ujao lazima uchague kipaumbele cha kitu ambacho unataka kukifanya kisha kisimamie kwa nguvu na muda mwingi, pata mida wa kukiwaza kitu hicho iwe kwa upande wa faida na hasara.

Chukua muda mwingi kukifikiria na kukitathimini kitu au kazi kama ndiyo haswa unayodhani itakutoa katika maisha yako kama Bakhresa alivyotolewa na biashara ya chakula, au kama Marehemu Kanumba alivyotambulika kwa kucheza filamu, kama Mwanamuziki Saida Karoli alivyochambuka kama karanga na kufahamika duniani kote, kama Mchezaji Messi anavyotambulika kwa kukiputa uwanjani, kama, Msanii Darassa alivyo kuja juu na Wimbo wa Muziki na wengine wengi.
Kaa chini orodhesha vitu vyote unavyovipenda kuvifanya kisha kwa mfano mimi napenda kufanya biashara ya kilimo, ufugani, duka, mama lishe na kuimba.
 
Ukimzaliza kuorodhesha pata muda wa kuvipiti vitu hivyo ulivyoviorodhesha mara kwa mara ili kujiaminisha kama ndiyo ambavyo unavihitaji katika maisha yako, je, ni kweli unahisi umezaliwa kufanya viti hivyo ulivyoviorodhesha au umeiga?

Ukipata orodha kamili ya vitu hivyo kwa mfano labda umepanga kufanya mambo matano katika maisha yako, mambo ambayo unaamini ukiyakamilisha basi maisha yako yatakuwa ya furaha hata kama HUTAPATA PESA LAKINI UNA AMANI YA MOYO. Hiyo ndiyo kazi au kazi ambazo unapaswa kuzifanya.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U

Itaendelea…………………………………………………………….
      edit