Nitakupa mfano mmoja wa zao la nyanya kipindi cha masika zao la nyanya
huwa linahitajika sana sokoni tena kwa bei nzuri, bei ambayo mkulima anaipanga
mwenyewe. Mkulima anapanga bei kwa sababu wahitaji ni wengi lakini wakulia
mwenye bidhaa ni wachache kwa sababu tu wengine walishindwa kukabiliana na
changamoto za kuivisha zao la nyanya.
Kwa kawaida kipindi cha masika magonjwa ambayo yanaliandama zao la nyanya
ni mengi sana ikiwemo ukungu, na mvua nyingi sana kama hutokuwa mvumilivu basi huwezi kutoboa
kwa zao hilo.
Lakini kama utafanikiwa kuivisha heka yako moja ya zao la nyanya katika
kipindi cha masika basi wewe ni mshindi utakuwa umepiga hatua nyingine, na
kipindi hicho ndicho haswa wakulima wenye kuthubutu hukitumia kupatia mafanikio
na ndiyo maana wakulima ni wengi lakini wenye mafanikio ni wachache.
Kwa wale ambao watalima nyanya nyingi katika kipindi cha kiangazi basi
ujue ni lazima wataangukia pua kwani nyanya sokoni zinakuwa ni nyingi kuliko
uwezo wa soko.
Kuwa kama mkulima wa nyanya za masika, chukua mfano huo wa mkulima wa
nyanya za masika kisha uvae uhusika wewe katika shughuli zako za kila siku,
kisha tumia fursa au nafasi inayopatikana kutengeneza pesa, ni lazima uwe wa
kitofauti tofauti, ni lazima uwe mjanja, mwenye kuthubutu.
Lazima uifanya akili yako kukubali matokeo makubwa sasa, kuyapa nafasi
mafanikio kwa kujituma na siyo kusema tu bila utendaji.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
MWISHO