Nilijitunza sana ili nisiuharibu mwili
wangu kwa kurukaruka na wapenzi tofauti.Niliamua kuishi bila mpenzi kwa muda
mrefu sana lakini mwisho niligonga mwamba kwa kaka mmoja ambaye ni mwenyeji wa
Arusha, mkazi wa Morogoro.
Ilichukua muda mrefu kumuamini na
kumkabithi moyo na mwili wangu. Nilihakikisha najiridhisha kwa kila hatua ili
nisije nikaangukia pua.
Nilimwambia naishi na mama pamoja na baba
yangu wa kambo, tukiwa tunaishi kwenye kijumba chetu cha tope kwenye kijiji kimoja
kilichopo mkoa wa Pwani.
"Kama kweli Maiko unanipenda basi
njoo nyumbani japo ujitambulishe ishu ya mahari siyo tatizo, naweza kuongea na
familia yangu wakatuelewa." Binti alimwambia Mpenzi wake.
Maiko aliniomba ajifIkirie kwanza kuhusu
hilo, je nini kilifuatia baada ya Maiko kufikiria? Usikose sehemu inayofuatia
ya mkasa huu kila Jumapili na Alhamisi saa 9 Alasiri.
Usikose
kesho muda kama huu hapahapa
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza
Hapa
Na: M&U.
NIMEAMUA KUJIUZA!-2
NILIPOISHIA WIKI ……
"Kama kweli Maiko unanipenda basi
njoo nyumbani japo ujitambulishe ishu ya mahari siyo tatizo, unaweza kuongea na
familia yangu watatuelewa." Binti alimwambia Mpenzi wake.
Maiko alikubali na kumwabia binti kuwa
atafikiria kuhusua suala hilo la kujitambulisha kwa wazazi wake.
ENDELEA NAMI……
Siku kadhaa zilipita huku tukiendela
kuwasiliana, Maiko akionesha ukaribu ambao nilizidi kumuamini, na mwisho wa
siku alikutana familia yangu akiwemo mama mzazi na baba yangu wa kufikia.
Walimkubaliana na kumpa utaratibu mzima,
alikubali na kuahidi kutekeleza kila kitu ikiwemo kutoa mahari.
Nilimwamini Maiko kama mwanaume wangu wa
pekee katika maisha yangu ambaye amejitolea kunipenda kwa dhati na ndiyo maana
ameenda hadi nyumbani kwetu kuzungumza na wazazi wangu, nilifurahi sana,
nilizidi kumpenda mno Maiko.
Sikuona sababu za kumbania kumpa tunda la
roho ingawa sikutaka kumuonesha kuwa niko tayari amege tunda langu, ila moyoni
nilimwamini na nilikuwa tayari kumpa utamu wangu, muda wowote na sehemu yoyote.
Hatimaye Maiko akapeleka kishika uchumba,
nikahisi sasa nimeishakuwa mke wa mtu, nikamkabidhi moyo wangu kijana Maiko.
Nakumbuka ilikuwa ni Jumamosi moja hivi
akaniomba tukutane Jijini Dar, nikakubali, nikawaga wazazi wangu kuwa naenda
kwa mwenzangu wakakubali.
Je, nini kilifuatia huko Jijini Dar
alikoenda kukutana na mpenzi wake, Maiko? Usikose sehemu inayofuatia ya mkasa
huu kila Jumapili na Alhamisi saa 9 Alasiri.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza
Hapa
Na:M&U.
@@@
NIMEAMUA KUJIUZA!-3
NILIPOISHIA WIKI…
Nilikutana na Maiko katika gesti moja iliyopo
maeneo ya Mabibo jijini Dar, tukafanikiwa kuanza uhusiano wa kimapenzi rasmi,
kama mtu na mchumba wake.
Nilitembea na Maiko mara kadhaa, hatimaye
nikaanza kuona mabadiliko katika mwili wangu kwanza sikuweza kupata hedhi,
nikawa najiuliza nimekuaje, nilikua sijui namna ambavyo mimba inaingia na kusababisha
hicho ambacho nilikiona kwangu.
Sikumwambia mama yangu mapema nilichofanya
nilijaribu kuwadadi wanawake ambao wananizidi umri, wengine walinielewesha
wengine walinishushua kuwa tayari nimenasa.
Niliendela na hali ile huku mwili nao
ukianza kubadilika, mara muda mwingi nikawa nahisi uchovu tu, nikilala mara
nageuka hivi mara vile ilimradi kero tu.
Mwisho wa siku ile hali ilinichosha na
nikaamua kumwabia mama ukweli, kuwa mimi mwanaye yatari nimenasa, mama
hakushangaa sana si unajua watu wa kijijini, basi aliniambia niwasiliane na
mwenzangu kuhusu taarifa hizo njema.
Nilifurahi sana moyoni mwangu kwani
niliona nitakuwa nimekamilika kuitwa mwanamke wa ukweli kwa kupata mtoto, na
tena mchumba wangu Maiko atanipenda sana kwa sababu huwa nasikia baadhi ya
wanawake ambao wanakuwa hawana uwezo wa ubeba ujauzito hunyanyasika sana kwa
waume zao na hasa mawifi mtu.
Niliamua kutoka pale kijiji hadi eneo la
center kwa ajili ya kumpigia simu Maiko kumfahamisha kile kilichotokea,
nilipopiga kwa mara ya kwanza simu yake ikawa inaita tu, nikapiga tena na tena.
Nikiwa nimeishaanza kukata tamaa na kuhisi
labda pengine mchumba wangu Maiko atakuwa kwenye matatizo, ghafla nikaona
amepokea, ila nikastaajabu akiniuliza swali ambali sikulitegema kulisikia
kutoka katika kinywa chaka hasa ukizingatia tulikuwa na muda mrefu
hatujawasilia.
Je,
unajua binti huyu aliulizwa nini na mchumba wake, usikose Siku ya Jumapili
kuanzia saa 9 alasiri.
Kwa USHAURI WA MAHUSIANO, MADA ZA MAHABA, HADITHI,
MACHOMBEZO, MIKASA YA KWELI YA MAPENZI NA UJASIRIAMALI. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza
Hapa
Na:M&U.
@@@
NIMEAMUA KUJIUZA!-4
NILIPOISHIA…
Nikiwa nimeishaanza kukata tamaa na kuhisi
labda pengine mchumba wangu Maiko atakuwa kwenye matatizo, ghafla nikaona
amepokea, ila nikastaajabu akiniuliza swali ambali sikulitegema kulisikia
kutoka katika kinywa chaka hasa ukizingatia tulikuwa na muda mrefu
hatujawasilia.
ENDELEA NAMI…
“Unasemaje” sauti ya Maiko ilisikika
upande wa pili ikiongea kwa jazba, jambo ambalo sikuamini, kwani nilizoea
kumsikia Maiko akiwa katika sauti nzuri, ya upendo na furaha.
Ghafla tumbo lilianza kunikata,
nilighafirika na kuamua kukata simu kisha nikaanza kumwaga machozi nikiwa pale kwa mwenye kibanda cha simu.
Alinishangaa sana Yule kaka ambaye alikuwa
anatoa huduma ya simu, akaniuliza nini ambacho kilikuwa kimenisibu, sikuweza
kumwambia kisha nirudi tu kijijini, siku
zilipita bila Maiko kunijulia hali, nishangaa sana hata mama yangu nahisi naye
alishituka kuwa pengine kutakuwa na kitu, alimua kuniuliza, vipi tena mwenziyo
mbona simuoni au hujamwambia kuwa una ujauzito.
Mama aliniuliza, nikamdanganya kuwa siku
ile niliyoenda center kumpigia simu hakuwa anapatikana hivyo nitaenda siku
nyingine.
Siku mbili zilipopita mama
alijichangachanga pesa kidogo aliyoipata kutokana na kufanya vibarua vya kuvuna
karanga kwenye mashamba ya watu wengine na kunipa ili nitumie njiani kama
nauli.
Nilifika hadi eneo la kibanda kile na
kuomba muda wa kuongea nikapewa,
nilimpigia Maiko alipokea kwa kana kwamba alikuwa ana hasira na mimi au
hakutaka kupokea simu yangu.
“Unasemaje. Mbona wewe msumbufu
sana,”alisema Maiko.
Nikabaki nashangaa leo hii mimi nimekuwa
msumbufu kwa Maiko, inakuaje, nikawa nahisi sijielewei elewi vile. Nilimwabia
Maiko samahani sana kama kuna jambo nitakuwa nimekukosea, ila nafahamu sijakosa
chochote.
“Haya sema haraka bhana mimi nina kazi
nyingi za kufanya,’ alinijibu.
Maiko, mimi sijisikii vizuri kwa sasa,
kabla hata sijamaliza alinidaikia jukwaju sasa mimi nifanyeje. Maiko nina mimba
yako, tangu siku ile ya mwisho tulipokutana faragha sikuziona siku zangu.
“Sikiliza Kecho, naona unataka kunizoea si
ndiyo, nani aliyekwambia anahitaji mtoto, kwa sasa mimi sijajipanga, cha
kufanya huyo mtoto chukua kama zawadi yako,” kisha akakata simu huku akiachia
bonge la mfyonzo.
Niliumia sana sikuamini kama nimeingizwa
kingi kirahisi hivyo na mbaya zaidi mimba juu, nilijiuliza ni kwa namna gani nitamwambia mama
yangu na anielewe, maskini mama alijitolewa kunipatia nauli ili nikaonane na
mtu ambaye aliamini ni muungwana, babamkwe wake lakini kumbe ni mtu katili.
Niliamua kurudi nyumbani huku nikiwa nalia
njia nzima, niliona kama nimejiabisha sana pale kijijini na kuwaabisha wazazi
wangu. Mbaya zaidi kuna vijana ambao walikuwa wananitaka lakini niliwakataa kwa
sababu tu ya Maiko.
Usikose kufuatilia nini kilifuatia baada
ya msichana Kecho kufika nyumbani kwao.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge Na M&U SMS
Au M&U Whatsapp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza
Hapa
Na:M&U.