Ikumbukwe kwamba katika utafutaji au utimizaji wa ndoto siyo tu kuwa na
pesa wakati mwingine kunahitajika ‘koneksheni’, rasilimali watu, mawazo na
pesa.
Kama una wazo zuri lakini mwaka huu ulishindwa kulikamilisha kwa sababu
ya kuhofia kudhulumiwa au kuingizwa mjini basi jitahidi upate elimu ya
kulithibiti wazo lisiibiwe na mtu mwingine lakini pia kumbuka kuwa uwoga wako
unaweza kuwa ndiyo umaskini wako.
Kama una vitu vyote kwa maana ya WAZO, WATU, PESA kwa nini hujaanza au
kama una kila kitu ila huna KONEKSHENI basi tengeneza njia za kupata koneksheni
mpya kila siku.
Kama wewe una wazo lakini hujui watu wa kuwafikishia basi jitahidi
kujikita katika kufikiria na kujifunza namna ya kupata koneksheni ya watu
mbalimbali.
Wengine wanashindwa kwa sababu tu hawako tayari kufuatilia, yani akienda
sehemu aambiwa kuwa nenda kaandike barua, kisha peleka kwa mjumbe, mwenyekiti
na mtendaji basi yeye anaona usumbufu huku akisahau kuwa hauna jambo jepesi
katika dunia hii.
Mwaka ujao uanze kwa mafanikio hasa kama utasoma makala hii na kuifanyia
kazi, usikubali kushindwa kwa sababu ya uzembe, uvivu, ulewena na mambo
mengine, pigana kuhakikisha unafahamu kile unachotaka kukifanya.
Dunia ya sasa ni ya utandawazi wakati mwingine elimu siyo lazima kwenda
darasani unaweza kuipata sehemu yoyote hata hiyo mitandao ya kijamii
unayoitumia inaweza kukusaidia kufanikisha jambo flani.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
Itaendelea…………………………………………………………….