Sunday, January 1, 2017

Published 1/01/2017 04:52:00 PM by

KAMA ULIKUWA HUJUI, MATATIZO HUZALISHA MAPENZI MAPYA





Nikukaribishe tena katika kupata chakula cha ubongo kwa upande wa Mahusiano, ambayo yamechukua sehemu kubwa ya maisha ya mwanadamu maisha yake ya kila siku.

Baadhi ya wapenzi ni kama vichwa maji, kila kukicha wao ni watu wa kuzua matatizo, mabala au kero mbalimbali pasipo kufahamu kuwa kero hizo zinazaweza kutoa nafasi kwa mchepuko kumiliki penzi lake.


Kero na gubu za kwenye mahusiano unaweza kuziona ni ndogondogo na za kawaida lakini kiuhalisi ni hatari na mbaya zaidi katika mustakabali wa penzi husika.
Kwani zinachosha, zinaboa, zinahuzunisha, zinasikitisha, zinakatisha tamaa na kadhalika. Nikupe angalizo wewe ambaye uko kwenye mahusiano ya kimapenzi, kiuchumba au mke na mume jitahidi sana kuwa mwerevu na mstaarabu kwani karaha na kero zako kwa mweza wako zinaweza kumuhamisha na kuanza kuanza kugawa penzi lako nje.

Kwa sababu tu kila akiingia kwako ni kero mtindo mmoja mara hivi mara vile, mwenzako ametoka kazini amevurugwa au amejichokea badala yaw ewe kumpetipeti lakini matokeo yake anaanza kufikia madeni ya vikoba, maneno maneno, matusi, kejeli na mengineyo.

Wewe endelea sasa ipo siki yatamshinda na wala hautaamini, siajabu akakuachia hata nyumba mliyojenga pamoja ilimradi tu aepukane na shari zako.
Mwanamke au mwanaume gani usiyekuwa na nidhamu katika kuzungumza na mwenza wako? Hata kama amekosa unaweza kutumia busara katika kutatua mgogoro wenu na siyo kupayukapayuka hadi majirani wanaelewa chanzo cha ugomvi wenu.


Kero zisizo na mipaka unaweza kuziona ni za kawaida lakini hizo ndizo zinazoanza kujenga usaliti na ufa katika ndoa yako, katika mapenzi yako. Ikitokea siku moja akapata mwanya wa kukutana na mchepuko na mchepuko huo ukaonesha kumpetipeti tofauti na wewe unavyomchukuliaga basi ujue imekula kwako.

Bila shaka hakuna mtu ambaye anapenda penzi au utamu wake ugawanywe kwa mwingine, kama wewe ni mmoja wa wale ambao hawapendi utamu wako aupate mtu mwingine basi badilika, tengeneza mazingira ya amani na mpenzi wako, jitahidi kuepukana na migongano isiyokuwa na maana dhidi yenu.

Jaribu kujichunguza na kubadilisha mwenendo wako mzima wa maisha ya kila siku katika mahusiano lasivyo kila siku utakuwa unalia kwa kuachwa, kila siku utakuwa unakorofishana na mwenza wako kwa kumfumania, kila siku utakuwa unakwazana na majirani kwa kuwahisi kutembea na mumeo.

Kwa tabia hiyo uliyonayo jaribu sana kuwa mtu wa tahadhali ili usisababishe kukwazika au kumkwaza umpendaye. Kama utajizuia kutomkwaza mwenziyo na yeye kutokukukwaza mtaishi kwa amani na upendo sana kwenye uhusiano wenu.
Pamoja na kuwa makwazo, gubu na changamoto za mapenzi ni ngumu kuziepuka lakini jitahidi kuziepuka kwa kukwepa migongano ya kusababisha , kuhisi na kufikiria.
Hii itakusaidia kuendelea kudumu kwenye uhusiano wako tofauti na unapokuwa kero kwa mwenza wako,  ni sawa na kukaribisha maadui au michepuko kwenye himaya yako.
 

Mada hii si kwa wanawake tu, kwani wapo pia wanaume wenye gubu na kero kwa wake zao. Unakuta kila akirudi jioni yeye ni mateke, vipigo kwa mpenzi wake hata bila sababu. Shauri yako na hiyo tabia ya ajabuajabu, utakuja kutorokwa na mkeo kuchukuliwa na kimshikaji ambacho ulikuwa unakidharau  lakini kanajua kubembeleza na kuishi na mwanamke vizuri, sasa kameamua kutumia madhaifu yako kukupokonya mke. Fanya marejeo mapya ili kudumisha na kuboresha uhusiano wako kuepuka kumegewa utamu wako.



Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
      edit