NAPENDA kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kukutana nawe tena katika uchambuzi wa makala
haya.
Mada ya leo inazungumzia
mtu ambaye ameachwa na mpenzi wake na akapata mpenzi mwingine lakini naye
akamuacha, akapata mwingine pia akaachwa, kwa nini iwe hivyo kila siku kwako tu
au tatizo nyota!
Zipo sababu nyingi sana
ambazo zinachangia wapenzi wengi kuachwa na kila mpenzi anayempata, wakati
mwingine unakutana naye mara moja mara baada ya kushiriki naye tu tendo la ndoa
mwenzio anatoka nduki, mazima!
Wanadamu wanashindwa
kutambua kuwa kila mmoja ana nyota yake, wakati mwingine ili muweze kudumu
kwenye uhusiano lazima nyota zenu zishabiiane na kama ikitokea sivyo ndivyo
basi kila siku uhusiano wenu unakuwa wa vimbwanga, ngumi, mateke, matusi,
kejeli mara kumwagiana maji ya moto, kusuruhishwa kwenye ofisi za serikali ya
mtaa, viongozi wa dini na hata familia zenu.
Kwa ufahamu wangu kama
nyota zitashabihiana mtakuwa mnakorofisha kiasi cha kuwashangaza majirani kuwa hamtoishi
pamoja lakini mwisho wa siku maisha yanasonga mpaka mmoja wapo anapoaga dunia.
Ila kwa nyota zisizoendana ni ngumu sana kustahimili katika mapenzi hayo.
Unaweza kukuta mtu ana
mpenzi wake kila siku ugomvi, matusi, maneno na vituko haviishi kila kukicha,
wakati huo mtu huyo huyo akapata mpenzi mwingine na wakadumu kwa muda mrefu na
hata ukiwaona mtaani ni kama marafiki, wanatembe kwa furaha, wanazungumza kwa
upendo na wanapokuwa faragha wanashirikina kwa vyote.
Haimaanishi kuwa wao
hawagombani, la hasha! wanagombana sana ila nyota zao zimerandana, wana
legalega ila sio kuanguka kama kwa wengine.
Ni dhahiri kila mtu
anakubali kuwa uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 uliokuwa na vuguvugu kubwa kwa
sababu ya wagombea wake ambao Dk. John Pombe Mgufuli na Waziri Mkuu mstaafu,
Edward Lowassa ambao kwa mujibu wa mnajimu, Maalimu Hassan Yahaya, nyota zao
zilikuwa hazishabihiani kwa maana mmoja ana nyota ya maji na mwingine moto
ambapo vitu hivi viwili havijawahi kupatana na ndiyo maana kiny’ang’anyiro cha
uchaguzi wao kilikuwa kikali.
Vivyo hivyo kwenye mapenzi
kama hakuna vitu ambavyo mnashabihiana basi linaweza kuwa ni seheme ya
kuchangia wewe kuchika au kuachwa na kila umpataye. Kikubwa mshukuru Mungu kwa
kila jambo na zungumza naye kuhusu kukupatia mpenzi mwema ambaye mtabarikiwa
kufikia ndoa.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Na.M&U