Wednesday, January 4, 2017

Published 1/04/2017 03:30:00 PM by

FANYA HIVI MWAKA 2017 KUFIKIA MALENGO YAKO-4




Kwa kuwa umeishapata kazi au biashara hizo basi zichambue kwa kuzipunguka kazi hizo kama ni tano basi punguza kazi au biashara 2 ambazo unahisi hazina mashiko sana kwako, ili uache zile zenye umuhimu zaidi.

Baada ya kufanya hivyo zipitie hizo kazi au biashara ambazo umazibakiza kisha jiulize mara mbilimbili kama kweli ndizo hasa ambazo unapenda kuzifanya kwa moyo mmoja hata kama ni usiku au kwa usumbufu wowote ule uko tayari kuzifanya bila kujali ni kisia gani una ingiza bali amani tu ya moyo wako inatosha.

Ukishapata kazi ya amani ya moyo wako fanya hivi: Kwa kuwa umeishaipata kazia au biashara ambayo unaamini ni furaha ya moyo wako basi jitahidi uanze kufikiria ni kwa namna gani kazia au biashara hiyo itakusaidia kuingiza pesa kwa namna yoyote ile. Mjasiriamali ni mtu ambaye anaweza kutoa jambo fulani lakini baadaya akatafuta sehemu yenye mwanya way eye kupatia pesa akautumia na kutengeneza pesa.

Kwa maisha ya Kibongo  huwezi kufanya kazi bila kuwa na maslahi hata hao watu wan je ambao tunaamini wanapesa nyingi kiasi cha kutupa misaada si kweli kwamba huwa watoa bure, wanajua ni sehemu gani watatumia kurudisha pesa zao.
 
Jifunze kutumia fursa, nilishafundisha kuwa kwenye matatizo ndipo hapo kwenye fursa, kikubwa ni kujipanga kutatua matatizo hayo ili wewe uingize pesa. Kwa kuwa ni pesa ambayo inakuwa imechanganyikana kwenye matatizo kuitoa kwa usafi ili iwe pesa kamili inahitaji nguvu, akili na muda wa ziada, ndiyo maana wengine hushindwa kuvumilia au kutumia fursa hiyo na matokeo yake huendelea kuwa maskini.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U

Itaendelea…………………………………………………………….
      edit