SOMO la leo lina lengo la kukuhimiza kujitahidi kufikia ndoto zako bila
kujali umefeli mara ngapi, umeachwa mara ngapi, umeumizwa au kupigwa mara
nyingi, yote hayo yachukulie kama changamoto katika maisha yako, lakini kwa mwaka
mpya wa 2017, haijalishi kama hukufanikiwa au la, kikubwa ni kujipanga kwa
kufanya mambo yale yale lakini kwa mbinu mpya.
Watu wengi wamekuwa wakitamani tu kupata pesa nyingi kwa haraka bila ya kuwa
na mipangilio madhubuti katika kuzitafuta au kutengeneza njia za kuzipata pesa
hizo. Kama wewe ni miongoni mwao basi badilika kupitia makala hii.
Kila mtu ana ndoto au malengo yake katika maisha, bila kujali ukubwa wa
ndoto au malengo kwani yanatofautiana kutoka kwa mtu mmoja na mwingine. Na
ndoto hizo hakuna anayeweza kukufanya uzifikie isipokuwa ni wewe mwenyewe kwa
msaada wa watu wanaokuzunguka.
Lakini kama utakaa na wazo lako ukisubiri mtu aje akusaidie ni sawa na
kufa bila kelele, kufa huku unajiona bila kujitetea, jambo ambalo kwa mtu
mwenye uchungu na ndoto, hayuko tayari kuvumilia misemo hiyo.
Kama umeharibu mwaka 2016 basi mwaka ujao unavyaoanza jipange mapema
zaidi, anza kwa kujiuliza kwa nini mwaka huu umefeli au umeshindwa kufikia
malengo au ndoto zako.
Orodhesha vitu vyote ambavyo vimesababisha ili mwaka ujao utakapoanza
kupigania ndoto zako uwe unafahamu namna ya kukabiliana na zile changamoto
ambazo zilikukwambisha mwaka huu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U