Thursday, January 5, 2017

Published 1/05/2017 12:00:00 PM by

ANANIHUDUMIA KILA KITU ILA SIYO MWAMINIFU





Naitwa Zay ni mwanamke wa miaka 25 , nilibahatika kupata mtoto kwa mwanaume ambaye baadaye aliniacha na nikaendela na maisha yangu mengine.

Baadaye nilimpata mwanaume mwingine ambaye niko naye kwenye uhusiano hadi sasa ingawa nahisi kwenye MAPENZI SINA BAHATI kwani mwanaume niliyenaye nshukuru ananipenda, ananijali na kunitunza sana lakini JAMAA SI MWAMINIFU mara kwa mara amekuwa akifanya makosa yaleyale ninayomkataza na kumsihi asiyafanye.

Ni mwanaume pekee ambaye niko naye kwa sasa ila ananiumiza sana kichwa pamoja na kunisaidia mimi binafsi na familia yangu pia anamsomesha mtoto wangu (ambaye yeye si mwanaye wa kuzaa) lakini sasa HATAKI NISHIKE SIMU YAKE, ANA UTANI MWINGI NA WADADA AMBAO WENGINE NAHISI KAISHA TEMBEA NAO.
 
Analipa kodi ya nyumba, ananisaidia kazini ninapokwamna na hivi karibuni amenishauri nirudi shule.
Wana M&U aombeni mnifungue akili katika ushauri wenu, kipi cha kufanya juu ya penzi na maisha yangu kwa ujumla?
 
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U

      edit