Wednesday, January 4, 2017

Published 1/04/2017 10:00:00 AM by

MUME WANGU HALALI NDANI NAPOKUWA KAZINI!


Nimeolewa na nina watoto 6 kwa mume wangu ambaye nilianza naye maisha miaka 12 iliyopita.
Mimi ni muuguzi katika hospitali moja iliyopo mkoani Kigoma, nimekuja kugundua kiutokana na majukumu yangu ya kufanya kazi zamu ya usiku nimegundua kuwa mume wangu huwa naye halali ndani, nikitoka kwenda kazini na yeye anatoka kwenda kwa mchepuko wake.

Baada ya kuhisi hilo niliamua kuweka mitego ili kuweza kumkamata na kuujua ukweli kama huwa anachepuka au lah.

MTEGO WA KITANDANI
Nilipoingia zamu ya usiku nikaweka mtego kwa kutandika kitanda kwa mtindo flani ili kama hatolala nijue, kweli mtego ule ulinasa, wangu hakulala nyumbani.


MTEGO WA SABUNI 
Mtego mwingine niliweka sabuni mpya bafuni ili kama akiamka si lazima ataoga lakini na yeyewe nikaikuta iko vilevile.


MTEGO WA UMEME
kuna siku nilinunua unity chache za umeme ili ikifika muda flani uzimike, kweli ukazimika usiku kesho yake nikamuuliza nasikia umeme jana usiku ulikatika akasema yeye hafahamu labda kama ulikatika usiku sana. Akasema yeye alirudi nyumbani saa 3 usiku akaingia kulala kwahiyo hakujua kitu.

Wakati huo dereva wetu wa boda×2 anadai hiyo saa 3 ya usiku anayosema alimuita sehemu akachukua pesa nakuondoka.
Hapa nilipo nina maumivu sana na kitendo cha mume wangu, nimejiridhisha je, nichukie hatua zipi?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Unaweza tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U
      edit