Mungu
wangu uliyeumba dunia na vitu vyake vyote vyenye kuonekana na visivyoonekana,
ninaomba uniongoze na kunisimamia katika maisha yangu mapya ya mwaka 2017.
Nimekuwa
nikiteswa na WACHUMBA FEKI, MADENI, KUFUKUZWA KAZI, KUDHARAULIWA, KUTENGWA,
KUSHINDWA NA MASOMO, MAPEPO/ MASHETANI, KUTOKUFIKIA MALENGO YANGU, MAGONJWA
SUGU NA HATA KIFUNGO KWA KUTOKUWA NA HATIA.
Nina
amini uhusiano wako na mimi BABA haukuwa mzuri MWAKA 2016 kushuka chini,
ninahitaji mabadiliko katika MATENDO, HISIA, MANENO NA WAJIBU. Lakini kwa MWAKA
2017 KUENDELEA UKAWE MZURI WENYE KUPENDEZA ZAIDI MACHONI PAKO.
Nafahamu
kama mwanadamu nimekukwaza, nimekudharaulisha, nimekufanya, uonekane si
mshindi, si mvumilivu, huwezi kuponya, huwezi kubariki, huwezi kufufua, huwezi
kufanikisha huwezi kufanya mtu akapata MKE au MUME MWEMA wakati huo ndiyo
WASIFU WAKO MUNGU.
Nimeteleza
nakuanguka mara nyingi katika maisha yangu chanzo kikiwa ni mambo ya kidunia,
shetani na kadhalika lakini MWENYEZI MUNGU hukuniacha kwa sababu ya upendo wa
kweli.
Naona
aibu machoni mwako MUNGU, natamani kurudi kama mwanzo ulivyonipulizia pumzi na
kunipa miliki za dunia hii, NIONGOZE BABA, NITAKASE MKOSEFU MIMI.
Uliweza
kunitoa kusikojulikana (Mafichoni) na kunifikisha hapa nilipo, nina IMANI
hakuna mwanadamu awezaye kunikweza isipokuwa ni wewe pekee.
Nimechoka
na UMASKINI katika maisha yangu, nimechoka na AFYA MGOGORO katika maisha yangu,
nimechoka KUISHI BILA AMANI YA MOYO KAZINI KWANGU, Nimechoka kukwazana na MPENZI,
MCHUMBA, MKE AU MUME WANGU.
Nifanye
upya mwanao, nahitaji rehema zako, nahitaji upendo wako wa awali, Nimechoka
KUTESWA kwa sababu ya MAPENZI na MAMBO YA WALIMWENGU.
Nina
kuomba baba katika jina na mwanao YESU KRISTO. AMINA!
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.
Pia
tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U